RPC RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
Na Stephano Mango,Songea
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamsaka mtu mmoja aliejulikana
kwa jina Methid Ndomba mkazi wa kijiji cha Liwale wilayani Mbinga kwa tuhuma ya
kumuua kwa kumkakata na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani John
Mapunda(35)mkazi wa kijiji hicho na kuutekeleza mwili wa Mapunda katika kati ya
bara bara ya kijijini hapo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema
kuwa tukio hilo lmetokea Agosti 3 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika
kijiji hicho cha Liwale ambako inadaiwa mwili wa marehemu Ndomba ulikutwa kati
kati ya bara bara ukiwa na majeraha makubwa huku damu zikiwa zimetapakaa kwenye
eneo hilo.
Kamanda Msikhela alifafanua kuwa chanzo cha tukio hilo
ulikuwa ni wivu wa mapenzi ambapo baada ya mwanamke mmoja ambaye jina lake
limehifadhiwa aliyedaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wawili hali
iliyosababisha kuqepo kwa ugomvi mkubwa kati ya wanaume hao uliopelekea kuwepo
na vitisho ambapo Ndomba inadaiwa kuwa aliwahi kumuonya marehemu Mapunda kwa
kumtishia kuwa endapo ataendelea kuwa na mahusiano na huyon mwanamke atamfanyia
kitu kibaya lakini Ndomba hakuweza kumsikiliza na aliendelea na mahusiano na
huyo mwanamke.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kuona kuwa Mapunda amepuuza
onyo hilo alilopewa ndipo mtuhumiwa Ndomba alipoamua kumvizia Mapunda na kuanza
kumpiga kwa kumkakata na kitu chenye kali kisha kumtemlekeza na kutokomea
kusikojulikana.
Aidha Kamanda Msikhela alisema kufuatia tukio hilo jeshi la
polisi mkoani Ruvuma linamsaka mtuhumiwa huyo na pindi atakapokamatwa
atafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu shitaka linamlomkabili.
Mwisho.
Chapisha Maoni