Na Gideon Mwakanosya-Songea
SIKU MOJA kabla ya kuanza
mtihani wa darasa la saba mwanafunzi wa shule ya msingi Safina wilayani Mbinga
mkoa wa Ruvuma Benedict Ndunguru (14) amekufa papo hapo baada ya kugongwa na
gari mda mfupi akitokea shuleni.
Akizungumza na Mtandao huu jana
mchana ofisini kwake kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Revocatus
Malimi alisema kuwa tukio hilo lilitokea septemba 8 mwaka huu majira ya saa 12
jioni huko katika kijiji cha Buruma wilayani Mbinga.
alifafanua zaidi kuwa
inadaiwa siku hiyo ya tukio huko katika
kijiji cha Buruma kwenye barabara inayotoka mbinga mjini kwenda Mbambabay
wilayani nyasa gari lenye namba za usajiri DFPA 1128 aina ya Toyota Hilux inayomilikiwa
na shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Wilayani Mbinga ambalo lilikuwa
linaendeshwa na Samwel Mwambipile (33) mkazi wa Mbinga mjini likiwa kwenye
mwendo mkali lilimgonga mtembea kwa
miguu Ndunguru na kumsababishia kifo papo hapo.
alisema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasi wa gari hilo ambapo
dereva alishindwa kuhumudu usukani na kusababisha kutokea ajali hiyo na jeshi
la polisi tayari linamshikilia dereva wa gari hiyo huku likiendelea kufanya
uchuguzi wa tukio hilo la ajali na baadaye ukikamilika atafikishwa mahakamani
kujibu shitaka linalomkabili.
MWISHO
Chapisha Maoni