MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia kesho mkoani Ruvuma ikiwemo kukagua na kuzindua mradi mkubwa wa uranium katika
mto Mkuju Wilaya ya Namtumbo na alahasiri atafanya mkutano wa kuwaaga wananchi
wa mkoa kwenye uwanja wa majimaji
Akizungumza na waandishi wa habari
jana ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema kuwa Rais
Kikwete atawasili Mkoani Ruvuma leo asubuhi kwa ndege na atapokelewa na
Viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa Dini na wananchi kwenye uwanja wa
ndege wa Songea
Mwambungu alisema kuwa mara baada ya
Rais Kikwete kuwasili na kusaini kitabu cha wageni ataelekea wilayani Namtumbo kwa
ajiri ya kutimiza wajibu wake wa kiserikali wa kukagua na kuzindua mradi mkubwa
wa uchimbaji wa Uraniam katika mto mkuju na kasha atarudi mjini Songea na
kufanya mkutano mkubwa wa hadhara wa kuwaaga wananchi baada ya utumishi wake wa
miaka 10
Alisema kuwa siku ya jumatano ambayo ni Octoba 21 Rais Kikwete atarejea Jijini Dar Es Salaam kuendelea na majukumu yake mengine ya kiserikali
“Nawaomba wananchi waliopo katika
maeneo mbalimbali mkoani humo wajitokeze kwa wingi kumpokea na kumsikiliza Rais
Kikwete kwenye uwanja wa Majimaji ambaye kimsingi ameutendea mambo mengi mazuri
Taifa na Mkoa wa Ruvuma”Alisema Mwambungu
Alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa
Ruvuma wamepata bahati kubwa sana ya kuagwa na Rais Kikwete ikiwa ni siku
chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Octoba 25 mwaka huu ambapo
wananchi watatumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura
MWISHO
Chapisha Maoni