NA STEPHANO MANGO
WAPIGAKURA wa majimbo ya Peramiho na Songea Mjini wamejitokeza
kwa wingi kwenye vituo vyao vya kupigia kura za Urais,Ubunge na Udiwani na
wengine wamekesha kwenye vituo vya misufini namba 1 na namba 2 vyao vya kupigia
kura kwa lengo la kuwahi foleni ya kupiga kura huku kasoro ndogo ndogo
zikijitokeza lakini bila kuathiri zoezi zima la upigaji kura
Akizungumza na waandishi wa habari Msimamizi wa Uchaguzi
jimbo la Peramiho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Vijijini, sisbert Valentine Kaijage alisema kuwa waliojiandisha kwenye jimbo hilo ni 67,334
ambapo idadi ya vituo vya kupigia kura ni 195
Kaijage alisema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi
ya mwaka 2012 wilaya ya Songea Vijijini
ina idadi ya wakazi 133024 na kwamba vifaa vya kupigia kura vilishaperekwa
kwenye vituo kwa wakati na changamoto ambayo imejitokeza kwenye vituo hivyo ni
baadhi ya watu ambao walijiandisha kwenye majimbo ya uchaguzi wakiwemo
wafanyakazi na wanavyuo nao kutaka kupiga kura
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi Jimbo la
Songea Mjini Emmanuel Kibona kuwa kumejitokeza kasoro za Askari Mgambo kutokuwahi
kwenye vituo vya kupigia kura, baadhi ya wanasiasa kuvaa sare za vyama vyao
hali ambayo ilitaka kuleta taaruki, makarani kuendesha shughuli polepole na
kusababisha wapigakura kulalamika
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura
kwenye kituo cha Shuleni A kata ya Likuyufusi Mgombea Ubunge wa Chama cha
Mapinduzi Jimbo la Songea Mjini Leonidas Gama alisema kuwa ameridhishwa na hali
ya upigaji kura kwani umekuwa huru na haki
Gama alisema kuwa tume imetenda kazi yake vizuri kwa
kuhakikisha vifaa vyote muhimu vya kupigia kura vimefikishwa kwenye vituo kwa
wakati na wapigakura wameanza muda muafaka kutumia haki yao ya kikatiba ya
kushiriki kupiga kura za ubunge, urais na Udiwani
Naye Mgombea Ubunge wa Ccm Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama
mara baada ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Chekechea namba
moja kilichopo katika kijiji cha Parangu nje kidogo ya mji mdogo wa Peramiho
alisema kuwa anaamini kuwa wananchi wanaendelea kupiga kura bila kuwepo kwa
usumbufu wowote
Mhagama alisema kuwa wananchi wameonyesha kuwa na imani
kubwa na tume ya uchaguzi kwani hakuna mahala ambapo kumekuwa na dosari
kutokana na uzembe au udhaifu wa tume hiyo hali ambayo inaendelea kuufanya
uchaguzi huo kuwa huru na haki
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Thabit Mwambungu alisema
kuwa mkoa wa Ruvuma una majimbo 9 na kwenye
majimbo yote 9 ya uchaguzi katika mkoa huo vifaa vya kupigia kura vilipelekwa kwa wakati
na wale wote ambao walithubutu kuhujumu uchaguzi huo walichukuliwa hatua kali
za kisheria
Mwambungu alisema kuwa katika Jimbo la Namtumbo kuna kata
mbili uchaguzi wa udiwani umeahirishwa kwa makubaliano na Tume ya Uchaguzi kutokana
na makosa yaliyojitokeza na wagombea wanafasi hizo kwenye kata hizo wamekubali
uamuzi huo na kwamba katika kata hizo kura ya ubunge na urais zinaendelewa
kupigwa huo
MWISHO
Chapisha Maoni