Emmanuel Ntobi
Mwenyekiti wa madiwani CHADEMA MANISPAA YA SHINYANGA.
Mwenyekiti wa madiwani CHADEMA MANISPAA YA SHINYANGA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI. TAMKO LA MADIWANI WA CHADEMA HALMASHAURI YA MANISPAA SHINYANGA. KUPINGA
AZIMIO LA KURUHUSU SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA RAFIKI SDO KUFANYA SHUGHULI
ZAKE KWA "MASHOGA" NA "MACHANGUDOA" KATIKA MANISPAA
YA SHINYANGA.
Mapema wiki iliyopita, wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na
Watanzania kwa ujumla, wamepatwa na sintofahamu kubwa, baada ya kusikia na
kusoma kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, kuwa baraza
la madiwani Manispaa ya Shinyanga limetoa ruksa kwa shirika lisilo la
kiserikali la Rafiki SDO kufanya“mradi tata”wa Makaka Poa “Mashoga” na Madada
poa “Machangudoa” katika Manispaa ya Shinyanga.
Katika kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Shinyanga
kilichofanyika Alhamis ya tarehe 7/4/2016. Kikao hicho kilichoitwa cha
“dharula”kilikuwa na ajenda moja tu ya kuruhusu ama la, shughuli za shirika
hilo kufanya kazi katika Manispaa.
Hoja
hiyo ilipitishwa kwa kuungwa mkono na madiwani / wajumbe kutoka CCM. Katika
kikao hicho Madiwani wa CHADEMA tulipinga kupitishwa kwa azimio hilo. Ifahamike
kuwa,Shinyanga ina jumla ya madiwani 22,CHADEMA 07, CCM 16.
Mosi,Madiwani wa CHADEMA katika Halmashauri ya Shinyanga, tulipinga
ndani ya kikao na tunaendelea kupinga
kwa nguvu zetu zote, azimio hilo la kuruhusu Shirika la Rafiki SDO, ambalo
linataka kufanya mradi wake pamoja na mambo mengine ni kutoa elimu ya kutumia vilainishi (mafuta
maalumu ya kutumia wakati wa kujamiina)
kwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao "Mashoga" na
kwa wanawake wanauza miili yao “Machangudoa
", kwa kigezo cha kupunguza maambukizi ya UKIMWI. .
Kwamba, tunapinga mradi huu kwa sababuhauendani kabisa na maadili,
mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na Mwafrika . hivyo mradi huu ni hatari
kwa kuharibu maadili na utamaduni wetu kuwahi kutokea Tanzania na Afrika kwa
ujumla.
.
Kwamba,
tunapinga mradi huu kwa sababu unapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977, na sheria za nchi yetu, hakuna mahali ambapo
kumetambuliwa uwepo wa watu wanaitwa "Mashoga" na
"Changudoa" kama ni makundi katika jamii yetu ambayo shirika hili
linataka kufanya nao kazi ya kuwasaidia.
.
Kwamba, tunapinga azimio hilo kwa sababu tunahisi kuna hali ya rushwa kwa baadhi ya madiwani wa
CCM katika kufikia azimio hili la kuruhusu mradi wa shirika la Rafiki SDO, huku
wakitambua mradi huo unakiuka Katiba, sharia za Nchi, maadili na
utamaduni wa Mtanzania, na kuchukua tamaduni za kimagharibi. Kama wawakilishi
walipaswa kupinga mradi huu kama hapo awali tulivyopinga pande zote.
Hivyo tunasema, hakuna uhusiano wa kilichoandikwa katika
muhtasari wa shughuli za shirika hilo na
uhalisia uliopo mtaani, kuwa shirika hilo limedai linatoa elimu ya ujasiriamali
kwa “Mashoga” na “Machangudoa” .
Tunahoji kama wanatoa elimu ya ujasiriamali,
Ni kwa nini iwe kwa mashoga na machangudoa tu? Ilhali yapo makundi mengine kama
ya akina mama, vijana, watu wenye ulemavu na wengine walio katika mazingira
magumu. Lakini pia, ni njia zipi ambazo wametumia kuwatambua walengwa wa
huo mradi hasa mashoga?Kwa nini wanaibagua jamii yetu kwa matendo ya hovyo?
Maswali haya ndiyo yanatupa majibu kuwa kuna ulakini katika shughuli za shirika
hili.
Mwisho,
Tunaitaka Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi ifanye haraka sana yafuatayo.
Mosi , tunamtaka waziri mwenye dhamana ( kwa maana ya serikali
kuu) kuingilia kati na kusimamisha mara moja shughuli za shirika la
Rafiki SDO, lisiendelee na kazi zake
katika manispaa ya Shinyanga. kwa sababu mradi huu umekwishakuwa na utata kwa jamii.
Kwamba, tunataka kufanyike uchunguzi wa kina, kujiridhisha juu ya malengo na maudhui ya shirika hili la Rafiki SDO na mradi wao
kwa jamii ya Tanzania.
Kwamba tuitaka TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina kwa baadhi ya
madiwani wa CCM ili kubaini, wapi wametoa msukumo wa kuvunja katiba,
sheria za nchi, Maadili na Utamaduni wa Mtanzania na kukiuka kiapo chao.
Madiwani CHADEMA kamwe hatutokubali kuona kizazi hiki cha
kitanzania kinanaharibiwa kwa sababu ya faida ya watu wachache na familia zao.
Mwisho kabisa tunawaomba viongozi wa dini mbalimbali,wanashinyanga
na watanzania wote kwa ujumla,wakiwemo, wandishi, kutuungamkono kupinga kwa nguvu zote vitendo
hivi ambavyo ni dhahiri vikiachwa
vitaharibu maadili na utamaduni wetu watanzania.
Mabadiliko Daima.
Asanteni,
Imetolewa leo, Alhamisi Aprili 14, 2016 na :
Emmanuel Ntobi
Mwenyekiti wa madiwani CHADEMAMANISPAA YA SHINYANGA.
Mwenyekiti wa madiwani CHADEMAMANISPAA YA SHINYANGA.
Chapisha Maoni