NA, STEPHANO MANGO, SONGEA
HALMASHAURI ya Wilaya ya
Songea Mkoani Ruvuma imetoa jumla ya Shilingi milioni 259.5 kwa ajiri ya
utekelezaji wa Ujenzi wa Maabara katika shule Sekondari 23 za Sekondari
zilizopo katika Halmashauri hiyo
Akizungumza kwenye kikao
cha Baraza la Madiwani lililofanyika juzi kwenye ukumbi wa Mikutano wa
Halmashauri hiyo Mkurugenzi wa Wilaya ya Songea Sigsibert Valentine alisema
kuwa Halmashauri inaendelea kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi
wa Maabara tatu kwenye kila shule ya
Sekondari wilayani humo
Valentine alisema kuwa
hadi kufikia desemba mwaka 2014 halmashauri yake ilikwishatoa fedha na vifaa
vya viwandani vyenye thamani ya shilingi milioni 259,582,239 kwa ajiri ya
ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara
Alisema kuwa fedha hizo
zimetumika kuwalipa mafundi na ununuzi wa vifaa vya viwanda ambavyo
vimekamilisha ujenzi huo na kwamba kilichobaki kwa asilimia kubwa ni ujenzi wa
miundombinu ya ma maabara na chumba cha maandalizi(Preparation room), kufunga
mitungi ya gesi na kupaka rangi majengo hayo
Alifafanua kuwa Sekondari
zingine zipo kwenye hatua ya mwiso wa ujenzi kwani zinamalizia ujenzi wa
maabara hizo kwa kufunga lenta na kupaua na tayari kwenye akaunti za shule
zimeshaingizwa fedha kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi huo haraka iwezekanavyo
Alizitaja Sekondari hizo
ambazo zinajengwa maabara tatu kwa kila sekondari kuwa ni Sekondari ya Nguruma,
Maposeni,Nalima, MagingoLipupuma na Gumbiro zikiwa ni sekondari za kata
wilayani humo
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Muhukuru Rajabu Mtiula
aliwataka Wakuu wa Idara waliopewa majukumu ya kuhakikisha ujenzi huo
unakamilika kwa hatua zote wasimamie vyema rasilimali zote zinazotolewa na
Halmashauri
Mtiula alisema kuwa kila
muu wa Idara anapaswa kutumia nguvu zake zote kuhakikisha ujenzi huo
unafanikiwa kwani licha ya kuwa ni agizo la Rais Jakaya Kikwete lakini ni
muhimu sana kwani ni ukombozi mkubwa kwa wanafunzi ambao kwa muda mrefu
hawakuwa na maabara za kujifunzia masomo yao ya Sayansi
MWISHO
Chapisha Maoni