KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WATU 3 wanaozaniwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa na
siraha inayodaiwa kuwa ni SMG pamoja na mapanga huku wakiwa wamejifunga
vitambaa vyeusi usoni walivamia kituo cha mafuta cha Jamuhuli Petrol felling
station kilichopa katika eno la mtaa wa kalanje mjini Tunduru mkoani
Ruvuma na kupola fedha taslim shilingi million 7 pamoja na simu mmoja ya
mkononi yenye thamani ya shilingi laki tisa na elfu themanini kisha walikimbia
na kutokomea kusiko julikana.
Akizungumza na
Tanzania Daima jana ofisini kwake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 na nusu usiku
huko katika kituo cha kuuza mafuta ya vyombo vya moto cha Jamuhuli Petrol
felling station cha mjini humo.
Alifafanua zaidi kuwa
inadaiwa siku hiyo ya tukio watu 3 wasiofahamika majina yao wala sura zao wakiwa na bunduki aina ya SMG
huku wakiwa na mapanga walivamia kituo hicho hc amafuta na kuwatishia kuwapiga Risasi wafanyakazi
wakituo hicho huku wakidai watoe fedha walizokuwa nazo na baadaye walifanikiwa
kunyang’anya fedha shilling million 7 pamoja na simu moja ya mkononi
Sumsang Gallaxy huku wamewaweka chini ya ulizi mkali wafanyakazi wa kituo cha mafuta akiwemo Nasri Salum(27)
mwenye asiri ya kiarabu ambaye alikuwa anakamiliasha mahesabu ya mauzo ya siku
hiyo.
Alifafanua zaid kuwa inadaiwa kuwa awali majambazi hao walifika
katika kituo hicho cha mafuta mapema kama wateja wengine wakiwa na gari ambalo
namba zake za usajili hazikuwezakufahamika mara moja na baada ya kuudumiwa
walienda kulipa pesa dirishani gafla walitoa bunduki 2 na kufyatua risasi mbili
hewani kasha kutoa mapanga na kuwatishia kuwauwa wafanyakazi wa kituo hicho
huku majambazi hao wakidai watoe fedha zilizokuwepo kwa wakati huo kwenye kituo
hicho.
Alisema kuwa
majambazi hao walifanikiwa kupora kiasi hicho cha fedha kasha walikimbia na
kutokomea kusiko julikana ndipo baada ya hapo wafanyakazi walikimbilia kituo
kikuu cha polisi kutoa taarifa ya tukio hilo.
Kamanda Msikhela
baada ya tukio hilo kulipotiwa polisi askali polisi walikwenda kwenye eneo la
tukio na kulifanyia uchunguzi wa kipolisi ambapo waligundua maganda
mawili ya lisasi yaliyotumika na walipoyafanyia uchunguzi ilibainika kuwa ni
risasi ya bunduki aina ya SMG.
Hata hivyo kamanda
Msikhela alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoni humu linaedndesha msako mkali
wa kuwasaka majambazi hao na amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuona umuhimu wa
kutoa ushilikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa zinazoweza kufanikisha
kuwakamata majambazi hao.
Mwisho
Mwisho
Chapisha Maoni