NA STEPHANO MANGO, SONGEA
WANANCHI wa kada mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu uteuzi,
uhamishaji na uenguaje wa wakuu wa Wilaya uliofanyika jana na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na kudai kuwa jambo hilo halikuwa muda muafaka kwa sasa
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa walisema kuwa
muda uliopo ni wa utekelezaji wa maagizo yake mengi ambayo ameyatoa siku za
nyuma hivyo kitendo cha kuwaachisha, kuhamisha na kuteua wakuu wa wilaya wapya
kutasababisha kutasababisha kutokutekeleza mipango kazi husika kwasababu wapya
watataka kujifunza majukumu yao na kuanza kutembelea maeneo yao ya kazi ili
waweze kuyajua na kuanza kupanga mipango yao ya kazi husika
Masumbuko Paulo akizungumza na Gazeti hili alisema kuwa
uteuzi na mabadiliko ni muhimu kisiasa lakini kufanya sasa sio muhimu kwa
sababu ya mipango ya zamani haitatekelezwa na hawa wapya kwani nao watakuja na
mifumo yao ya utendaji kazi
Paulo alisema kuwa
jambo hilo sio la kulifurahia hata kidogo kwani kila yanapofanyika mabadiliko
ya uongozi taifa linaingia katika hasara kubwa kutokana na uhamisho,utekelezaji
ambavyo wakati mwingine havina tija na hivyo kuendelea kufanya matumizi yasiyo
yasababu na kuwabebesha mzigo mkubwa wananchi
Kwa upande wake Isidoli Mdolino Nyati alisema kuwa
anampongeza Rais Kikwete kwa uamuzi alioamua kwani amezingatia vigezo kulingana
na hali halisi ya mazingira kutokana na changamoto za maeneo husika
Nyati alisema kuwa katika uteuzi huo umefanikiwa kuingiza
vijana kwa asilimia kubwa lakini pia amejaribu kuzingatia vigezo vya jinsia
kwani ile asilimia hamsini kwa hamsini pia imejitokeza kwa umakini mkubwa
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Askofu James(AJUCO)
Denis Mpagaze alisema kuwa uteuzi huo ni wa kisiasa kwasababu hayo yote
anayoyafanya ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa udiwani,ubunge na urais na
kwamba haona tija kwa sasa
Mpagaze alisema kuwa wapo wakuu wa wilaya ambao walikuwa
wanajihusisha na harakati za watu waliotanga nia ya kutaka kugombea ubunge au
urais wamefutwa kazi na wengine wamehamishwa kwa lengo la kudhoofisha kambi
husika za kisiasa na kutengeneza ulinzi wake mara baada ya yeye Rais kuondoka
madarakani
MWISHO
Chapisha Maoni