KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MWALIMU wa Shule ya Msingi Kaijere iliyopo katika kijiji cha
Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Shaib Niali(30) amekutwa amekufa
huku akinin’ginia kwenye kenchi ya nyumba yake baada ya kujinyonga kwa kutumia
kanga
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo
zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela zilisema
kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane usiku kwenye chumba chake
alichokuwa analala
Msikhela alifafanua zaidi kuwa inadaiwa Niali saa moja usiku
kabla hajajinyonga alimpigia simu dada yake Asia Niali Mkazi wa majengo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kumjulisha kuwa anaumwa sana na alimuomba
aende haraka kijijini Namabengo akamuone na kisha ampeleke nyumbani kwa mama
yake mzazi alioko katika kijiji cha Lusewa
Alifafanua kuwa inadaiwa Niali kwa muda mrefu alikuwa ana
ugomvi mkubwa na mke wake ambaye baadaye walilazimika kutengana lakini Niali
alionekana kutokubali kukaa na watoto jambo ambalo lilikuwa linaleta ugomvi wa
mara kwa mara
Alisema kuwa Niali wakati anampigia simu dada yake ya
kumtaka afike kumuona Namabengo tayari alikuwa ameandaa kanga ya kujinyongea na
panga kwa lengo la kutaka kwenda kumcharanga mke wake ambaye anaishi mbali
kidogo na nyumba yake
Alieleza zaidi kuwa muda mfupi baada ya dada yake kupigiwa
simu na kaka yake, Asia aliwasiliana na
majirani wanaoishi na Niali usiku huo ili kujua kinachomsibu kaka yake, ndipo
majirani wakaenda nyumbani kwa Niali na kumkuta akiwa amejinyonga na kwamba
majirani hao waliwasiliana na Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Namabengo na
taarifa ikapelekwa kwenye kituo cha Polisi cha Wilaya ya Namtumbo
Msikhela alieleza kuwa Askari Polisi walipopata taarifa ya
Tukio hilowalienda haraka kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na Daktari
ambaye ndiye ayethibitisha kuwa Mwalimu Niali amekufa kwa kujinyonga kwa kanga
na kwamba upeleleza wa tukio hilo unaendelea
MWISHO
Chapisha Maoni