![]() |
HILDA AKIWA AMEJERUHIWA na wananchi wanaomwita mchawi |
![]() |
mauruci akigugumia maumivu baada ya kichapo |
WAWILI WAJERUHIWA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA PERAMIHO
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida watu wawili wakazi wa Kijiji cha
Muunganozomba kata ya Kilagano Peramiho wamechezea kichapo kikali kwa kutumia
malungu,panga na fimbo na kuwasababishia majeraa makali kwenye sehemu
mbalimbali za miili yao na kulazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Songea
Uchunguzi uliofanya na Gazeti
hili umebaini kuwa watu hao wamecharazwa bakora, panga na virungu kwa madai
kuwa wamemficha mtoto aliyefahamika kwa jina la Adam Mselewa(4) katika
mazingira ya kutatanisha yaani kiushirikina katika kijiji hicho
Tukio hilo lilitokea juzi kijijini hapo ambapo kundi la watu ambao
wanasadikiwa kuwa ni wana ukoo liliwashambulia Hilda Johnfan Pili(79) ambaye
amejeruhiwa vibaya kichani, mguu wa kulia na jicho la kushoto na Maurusi Zenda(
46) aliyejeruhiwa vibaya kichwani na mkono wa kushoto kutokana na kipigo
walichokipata
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela ili aweze kunipa kinagaubaga wa tukio hilo la kinyama na kusikitisha
kutokea katika eneo hilo na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa tukio
hilo
Akizungumza na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihaya
Msikhela alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba watuhumiwa kumi wamekamatwa kutokana na tukio
hilo na aliwataja watu hao ambao
wanadaiwa kushiriki kuwa ni Ambros
Mselewa(24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda(45) Lameck
Zenda(22) Pautas Komba(24) Fredy Mende(24)Gerord Ngonyani(27)Odilo Mwingira(21)
Shadrack Ngonyani(22) Hilda Zenda(36) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha
Muunganozomba
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya 1;00 asubuhi
huko katika Kijiji cha Muunganozomba ambako watu wawili walinusurika kuuawa
baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia
sheria mkononi kwa madai ya kushoshwa na vitendo vyao vya kishirikina
Alifafanua zaidi kuwa Inadaiwa chanzo cha tukio hilo ni kupotea kwa
mtoto Adam katika mazingira ya kutatanisha Kijijini hapo tangu Februari 3 mwaka
huu ambako Baba mzazi wa mtoto huyo Ambros Mselewa akishirikiana na baadhi ya
watu ambao walikuwa na hasira kali waliwavamia watu hao wawili na kuanza
kuwashambulia kwa madai kuwa wamemficha mtoto Adamu kwa mazingira ya uchawi
Alisema kuwa Polisi baada ya
kupata taarifa ya tukio hilo wakiwa wameambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa
walifika kwenye eneo la tukio mara na kuwakuta watu hao wawili wamejeruhiwa
vibaya na jitihada za kuwaokoa na kuwapeleka katika Hospital ya Mkoa wa Songea
ili wapatiwe matibabu
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Hilda Johnfan Pili(79) ambaye
amejeruhiwa vibaya kichani, mguu wa kulia na jicho la kushoto na Maurusi Zenda(
46) aliyejeruhiwa vibaya kichwani na mkono wa kushoto kutokana na kipigo
walichokipata
Alieleza zaidi kuwa kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi linatoa wito
kwa wananchi wote kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi na
badala yake wanapokuwa na watuhumiwa wahakikishe wanawapeleka kwenye vyombo vya
dola
Kwa upande wake Daktari Mfawidhi wa Hospital ya Mkoa wa Songea
Benedicto Ngaiza alithibitisha kupokea majeruhi hao na kwamba wamelazwa katika
Hospital hiyo kwa ajiri ya matibabu na mara hali zao zitakapoimarika
wataruhusiwa kurudi majumbani mwao
MWISHO
Chapisha Maoni