Rais Jakaya Kikwete akiwa na Lowassa kwenye moja ya mikutano ya kisiasa
NA,STEPHANO MANGO,SONGEA
JUMAPILI februari mosi Mwaka huu majira ya Saa tatu asubuhi
nikiwa nimeambatana na waandishi wenzangu wa habari kutoka vyombo mbalimbali tulikuwa
kwenye maeneo ya uwanja wa ndege wa Songea Mjini kwa ajiri ya kuwapokea
Viongozi Mbalimbali waandamizi wa chama na Serikali
Nikiwa uwanjani hapo na wenzangu nawaona watu wakiwa
wamesimama makundi makundi wakiwa wanazungumza mambo kadha wa kadha huku
wakipanga mikakati ya kuwapokea viongozi wao ambao walikuwa wanakuja kwa ajiri
ya Maadhimisho ya miaka 38 ya Chama cha Mapinduzi ambayo Kitaifa yamefanyikia
Mkoani Ruvuma Katika Uwanja wa Michezo wa Majimaji
Nikalisogelea kundi moja wapo ili kutaka kujua wanajadiliana
nini Uwanjani hapo, kumbe yalikuwa ni mazungumzo ya kuwapokea viongozi wao
lakini kubwa lilikuwa ni shauku ya kumuona Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Monduli Edward Lowassa
Sikuchelewa kudadisi kwa mmoja wa Mshiriki wa Kundi lile
ambaye alitambulika kwa haraka kwa jina
la Hamis kutoka Wilaya ya Namtumbo, nilipomuhoji kulikoni mbona wanashauku ya
kutaka kumuona Mbunge wa Monduli kuliko viongozi wengine waandamizi wa chama na
Serikali
Jamaa akanijibu kuwa Makundi yote haya unayoyaona hapa
uwanjani tunashauku ya kumuona Rais ajaye na tunataka kumwambia asife moyo na
changamoto ambazo anakutana nazo ndani ya chama kwa sasa kwani wao wanampenda
na wanaimani naye
“Leo tunahamu sana ya kumshangilia Mpendwa wetu Lowassa
kwani kwa muda mrefu ajaigusa ardhi ya Mkoa wa Ruvuma na kwamba Viongozi
wengine ambao wanafika Leo sio wageni kwani ni mara kwa mara wanafika na hakuna
wanachokifanya zaidi ya kumaliza fedha za wananchi kwa kigezo cha ziara huku
maamuzi wanayoyatoa hayatekelezeki”alisema kijana yule
Kijana yule nilizungumza nae mambo mengi sana yenye busara
na hekima kuhusiana na mchakato mzima wa kuwapata wagombea wenye kukubalika
miongoni mwa jamii wa ngazi zote za uwakilishi kwa maana ya Udiwani, Ubunge na
Urais mpaka ndege inashuka uwanjani ndipo tulipoachana kwa kupeana namba za
simu ili muda mwingine tuwe tunasalimia na kujadiliana mambo muhimu nchini
Niliachana na Kijana yule na kuwafuata waandishi wenzangu
ili tupate maelekezo ya watu wa Itifaki namna ya kuweza kupata matukio muhimu
uwanjani hapo, mara ndege inashika ardhi ya Mkoa wa Ruvuma na inatafuta uelekeo
wa egesho lake ili iweze kushusha abiria waliokuwamo ndani ya ndege hiyo
Wakati tunajipanga Kuangalia wanaoshuka ndani ya ndege hiyo
tuliona watu wachache wakishuka na mwisho akashuka Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa huku akipunga mikono na kuwafanya watu
waliokuwepo Uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe na vigelegele hali iliyomfanya
asalimiane na watu hao huku akitafakari na baadae msafara wake ukaelekea eneo
la maadhimisho
Wanahabari tuliambatana naye tukiwa na viongozi wengine
kuelekea katika uwanja wa Majimaji ili tuufikishe msafara wake na kurudi tena Uwanja
wa ndege ili kuwapokea wageni wengine kwani hata Mgeni Rasmi wa Maadhimisho
hayo ambaye ni Mwenyekiti wa Ccm na Rais Jakaya Kikwete alikuwa bado hajawasili
Wakati Tunaingia Uwanja wa Majimaji Mshereheshaji wa
Shughuli hiyo ya Maadhimisho kwa jina maarufu ni MC ambaye alitambulika kwa
Jina la Nyakia Ally ambaye ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi alipoutambulisha
Msafara wa Lowassa na kusababisha pia watu waliokuwepo uwanjani hapo
washangilie mpaka Lowassa anashuka ndani ya gari.
Mara baada ya Kushuka ndani ya gari Lowassa alilazimika
kuwapungia mikono kushoto na kulia watu waliopo Uwanjani hapo huku akiachia
tabasamu na kupunga mkono kushoto na kulia na kushangiliwa kwa vigelegele na
vifijo na kuelekea Jukwaani kwa kupanda ngazi kwa kukimbia kwa ajili ya kupata
nafasi yake ya kukaa ili aweze kuwapokea Viongozi wake wa Chama na Serikali
Sie Tulirudi tena Uwanja wa Ndege kumpokea Rais Na wageni
wengine walioambatana nae na kurejea tena uwanjani hapo tukiambatana na
Viongozi wengine waandamizi wa chama na Serikali wa Mikoa na Taifa na kwenda
nao Ikulu ndogo ya Songea kabla ya kuingia kwenye uwanja wa Maadhimisho ya
miaka 38 ya Chama hicho.
Mara baada ya Rais Kuingia uwanjani hapo ratiba iliendelea
kama ilivyopangwa na mamlaka zinazohusika lakini cha kushangaza sio Katibu wa
Itikadi, Siasa Na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa Ccm Abrahamu Kinana,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho Dkt Emmanuel Nchimbi na Mwenyeki wa Ccm
Rais Kikwete ambaye alithubutu kutambulisha Makada wa ngazi ya Kitaifa
waliokuwepo ndani ya Uwanja huo
Makada hao waliokuwepo kwenye Maadhimisho hayo ni wale ambao
wametangaza nia ya kuwania kiti cha urais mwaka huu ni Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
KImataifa Benard Membe, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchemba, Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na Stephen Wassira waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Kitendo cha kushindwa kutambulishwa Lowassa ambaye ni Waziri
Mkuu Mstaafu pekee aliyehudhulia
maadhimisho hayo kimetafsiriwa na wengi kuwa ni mkakati maalumu
ulioandaliwa na maafisa usalama baada ya kuona upepo wa shangwe alipokuwa
anashuka uwanja wa ndege na alipoingia ndani ya uwanja wa maadhimisho
Lowassa alipoingia Uwanjani hapo alikaa safu ya viti vya
nyuma kabisa akifuatilia kwa umakini hotuba mbalimbali za Viongozi Ikiwemo
hotuba ya Rais na mara baada ya Rais Kumaliza Hotuba yake na Mshereheshaji
kumuinua mwanamuzi Diamond ili aweze kuburudisha wananchi waliohudhulia
maadhimisho hayo
Watu wakiwa wanaendelea kumshangilia mwanamuziki huyo Lowassa
alishuka jukwaani akatokea geti dogo lililopo chini ya jukwaa na kuondoka eneo
hilo kabla Rais ajamaliza shughuli za maadhimisho hayo ikiwemo kukabidhi kadi
kwa wanachama wapya wa Ccm, kukabidhi hundi ya Malipo ya Epz kwa Meya wa
Manispaa kwa ajiri ya wananchi wa Kata ya Mwenge Mshindo
Kitendo cha wananchi kumshangilia Lowassa na Viongozi
kushindwa kumtambusha kimenifanya nifikirie upya na kwa umakini na niandike
makala haya ili wadau waweze kufanya tathimini katika mwenendo mzima wa
mchakato wa kisiasa nchini na hasa katika wakati huu mgumu wa kupata Serikali
ya awamu ya Tano
Rafiki yangu mmoja ambaye anafanya kazi Idara ya Usalama ya
Taifa Mkoa wa Ruvuma nilipozungumza naye aliniambia kuwa Kitendo cha Lowassa
kushangiliwa vile kinaonyesha namna alivyokuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa
makundi ya rika yote na makundi hayo
yanamtaka Lowassa awe Rais wao ajaye na ndio maana hakutambulishwa kwani
angetambulishwa uwanja mzima ungeripuka kwa shangwe na nchi nzima ingejua kwa
sababu Redio na Televisheni zilikuwa zinarusha matangazo hayo hali ambayo
ingeonekana kabisa kuwa chama kinampigia kampeni
Kitendo cha Lowassa kuondoka Uwanjani hapo kabla ya Rais na
Viongozi wengine kutoka kwa kutumia mlango wa dharura kulinusuru kuharibu
maadhimisho hayo kwani Makundi mbalimbali yalikuwa yanajipanga kumshangilia na
kumshika mkoni ili iwe faraja yao katika kinyan’ganyiro cha Urais mwaka huu
Kutokana na hali hiyo ni lazima tuanze upya kwa kutafakari
shangwe zile za Lowassa zinaleta picha gani kwa Taifa na jamii kubwa kuhusu
muelekeo wake wa Kugombe Urais kama tunataka kufikia malengo yetu kama Taifa
kwani kuanza upya huko kutaleta picha katika miaka 10 ijayo
Bila Kificho Lowassa ana kila aina ya sifa ya kuwa Rais wa
Serikali ya awamu ya Tano kwani mara kadhaa ameonekanakukubalika kwenye makundi
mbalimbali ya kijamii, kuelezea namna ya utatuzi wa changamoto mbalimbali za
kitaifa
Watanzania tunayo njia ya kuelekea kwenye maendeleo ya kweli
na njia hiyo ni Lowassa hivyo tunawajibika kuanza kufikiri na kujiandaa ili
tuwe na uhakika wa ujenzi mpya wa Taifa letu litakalokuwa na sura tofauti
kiuchumi,kijamii na kisiasa hapo kesho kwasababu kesho inategemea leo imeiandaaje
kesho
Tufanye kitu cha maana leo ili kiweze kuleta usalama na ustawi
kwa maaendeleo ya Taifa letu kesho na hapa cha muhimu tunachopaswa kujua ni
kitu gani cha kufanywa kwa uhakika bila kubahatisha ili kuweza kuleta matokeo
chanya
Lowassa ameanza kazi kubwa na inahitaji gharama na
itakayochukua muda wa miezi nane hivyo watanzania ni lazima tuthubutu kuanza
nae safari mpya ya ukombozi wa Taifa letu ambalo kwa sasa linakabiliwa na
changamoto nyingi sana
Ni lazima tuanze leo kwani tukiacha hadi kesho huenda
tukachelewa katika mapambano hayo, tusikubali matokeo mengine bali ni ushindi
wa jumla kwa jumla kama Taifa kwani wanashinda wale ambao wanaamini na
wamejiandaa kushinda
Tukichukua hatua hatua ya kwanza leo na kuendelea kuchukua
hatua ni dhahiri tutafika tunakolenga kufika katika kujenga taifa lenye sura
mpya, lenye tija kwa kizazi hiki na kizazi kijacho hivyo tuchukue hatua sasa
kujenga Taifa moja lenye nia moja na mstakabali mmoja
Tushirikiane pamoja kuipa nchi yetu nguvu mpya, dira mpya na
mwelekeo mpya kitendo cha Lowassa kutangaza nia ya Kugombea Urais kimetusajiri
rasmi katika mashindano mazuri ya kujenga taifa letu na katika hilo kushinda ni
lazima kwani sharti muhimu la mashindano yoyote duniani ni ushindi
Ni muhimu watanzania tukamtafakari mpya Lowassa kwani ndie
kiongozi pekee ambaye anaweza kuzikabili na kuzishughulikia changamoto za
maendeleo kwa ujasiri na mkazo kutoka ndani yake na kuliunganisha taifa hili
likawa lenye umoja na mshikamano
Kufikiri upya kutatupa mwanga mzuri wa kushikamana na
Lowassa katika harakati zake za kuwania Urais kwani rekodi zake za utendaji
ziko wazi na hiyo ndio nguzo yake kuu kwani ajasimama bila nguzo hivyo nguzo ni
yale ya nyuma
Watanzania tukiamua tunafanikiwa kuitunza vyema tunu hiyo
muhimu katika taifa letu kwani tunahitaji kuvuka salama katika uchaguzi wa
mwaka huu hivyo bila kumpata kiongozi mwenye maamuzi magumu katika utendaji
Taifa litayumba na kukosa muelekeo
Tunahitaji Kiongozi mwenye sifa kama za Lowassa kwani
atakuwa mvumilivu siku zote bila kuchoka wala kukata tamaa mpaka malengo
yatimie kwa manufaa ya waliomchagua kwani anatambua raha kupata ushindi katika
mazingira magumu
Naamini kwamba tutafika pale kwenye kilele cha mafanikio
kama tutafuata niliyoyasema kwa kuamua,kudhamiria na kutenda yaliyo chanya
wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi ambao utaifanya nchi iweze kujengeka
upya kisera na kiutendaji
Hakika Lowassa ni Kiongozi bora anayejari utawala, utu wa watu,
haki zao, maslahi yao na usawa kati yao na asiyewatenga watu kwa matabaka wala
kutengeneza madaraja katika jamii anayoiongoza na ndio maana katika uongozi
wake katika serikali aliweza kusimamia vyema yale ambayo aliona yana maslahi
makubwa kwa nchi bila kuteteleka na mafanikio yake tunayaona leo
Lazima tujenge upya tafakari zetu mwaka huu tukiongozwa na
dhamira njema na kuziweka pembeni fitina, chuki, matusi na vurugu kwa viongozi
wetu ambao tunaamini kuwa viongozi wazuri wanatoka kwa mungu hivyo ni lazima
tutangulize maslahi mapana ya nchi yetu
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana kwa 0715-335051
Baruapepe;stephano12mango@yahoo.com
Chapisha Maoni