0

MBUNGE WA PERAMIHO JENISTA MHAGAMA AKISISITIZA JAMBO

NA STEPHANO MANGO,SONGEA
Top of Form
  
MBUNGE wa jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu wa Bunge ,Jenista Mhagama amewataka viongozi wa  Jumuiya  za Wazazi,Vijana na Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kutoka chama cha  Mapinduzi(Ccm) kuhakikisha wanafanya kazi ya kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuipigia kura katiba pendekezwa ili kutoa fursa ya upigaji kura kwa wananchi  wengi katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.

Wito huo umetolewa jana wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Jenista Mhagama kupata nafasi
 mpya ya  kuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge  iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Parokia ya  Bombambili  Manispaa ya Songea  na kuhudhuriwa na viongozi wote wa
 jumuiya za chama  hicho.
 
Bottom of Form
Top of Form
Alisema kuwa pamoja na mambo yote ya maendeleo yanayofanywa na serikali inayongozwa na Ccm kazi iliyobaki katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ni kuhakikisha wananchi wanajiandikisha kwenye daftari la kupigia kura pamoja na kuipigia kura katiba pendekezi.

 Jenista alieleza zaidi kuwa kama viongozi wa jumuiya za chama hicho watasimama kidete kuhamasisha kwa wingi wananchi  kwenda kujiandikisha kwenye  daftari hilo ,itatoa fursa kubwa kwa wapigakura kushiriki kazi hiyo na hatimaye kukifanya chama hicho kuendelea kushika dola .
 “Ili chama chetu kiendelee kushika dola ni lazima viongozi wa chama toka kwenye jumuiya zenu kuinuka kwenda kufanya kazi ya kuhamasisha wananchi waende kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupigia kura  na si vinginevyo kwani vitambulisho vya kupigia kura vya zamani  havitatumika na msidanganywe na wanasiasa wa maji taka‘’alisema Waziri  Jenista.

Aidha Waziri  huyo licha ya kutoa maagizo hayo aligawa Baiskeri 19 zenye thamani ya shilingi milioni 2.2 kwa jumuiya ya wazazi ikiwa ni mwendelezo wa  ahadi zake ambapo tayari alishagawa baiskeli hizo kwa jumuiya zingine za  vijana na UWT kwa kila kata za jimbo lake .

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Songea vijijini Rajabu Uhonde akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya mgeni rasmi Jenista  Mhagama kuzungumza na wanajumuiya hao alisema kuwa chama chake kimejipanga vizuri kuhakikisha maagizo yote yaliyotolewa  toka ngazi ya taifa yanafanyiwa kazi kwa utekelezaji na aliwaonya wale wote ambao wameonesha  nia ya kutaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi  mkuu ujao wasubiri mpaka muda utakapo fika vinginevyo watachukuliwa  hatua za kinidhamu ndani ya chama.

Nao viongozi wa jumuiya hizo huku wakimshangilia Mbunge huyo walisema kuwa wao hawafikirii kuchagua mtu mwingine kwa kuwa aliopo anatosha kwa madai kuwa kawaletea maendeleo mbalimbali katika jimbo laozikiwemo  barabara ambazo zilikuwa hazipitiki katika vipindi vya nyuma ,elimu toka shule za sekondari 3 hadi kufikia 28,zahanati pamoja na  ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na kuongeza idadi ya walimu 349  waliopo sasa.
MWISHO.
Bottom of Form

Chapisha Maoni

 
Top