0



MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA SONGEA CHARLES MHAGAMA

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa  ya Songea  mkoani Ruvuma wamepitisha bajeti ya sh. 41,886,830,984 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato katika kipindi cha mwaka 2015 /2016.
 
Akisoma bajeti hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika janakwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ya manispaa ,Mchumi wa  manispaa hiyo, Raphael Tumain Kimary alisema kuwa mchanganuo wake unatokana na vyanzo vya mampato vya ndani vya halmashauri hiyo kiasi cha sh3,259,613,000.
 Alisema kuwa mishahara ni sh. 24,710,969,400, matumizi mengine toka serikali kuu sh.2,296,844,000 ambapo ruzuku ya miradi mbalimbali yamaendeleo sh.11,619,404,584 na vyanzo vya ndani vya halmashauri hiyo ni sh.3,259,613,000.

 Kimary  alifafanua zaidi kuwa vipaombele vya halmashauri hiyo ni kukamilisha miradi viporo ya majengo katika zahanati na vituo vya afya,ukarabati wa ofisi kuu ,kata na mitaa,ujenzi wa vivuko vya madaraja,sekondari,shule za msingi,pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu
 Mchumi huyo alivitaa vipaumbele vingine kuwa ni kuboresha mitandao ya barabara kwa kiwango cha lami kwenye kata mpya ambazo zimeongezwa  ili ziweze kupitika kwa urahisi hasa  kwa kata ambazo zipo mbali na makao makuu na manispaa hiyo na kuendelea kutekeleza mpango wa serikali wa tekeleza sasa kwa matokeo makubwa katika sekta ya kilimo,elimu ,maji pamoja na mapato.
 Kwa  upande wake meya wa manispaa hiyo Charles Mhagama mara tu baada ya madiwani wote kuridhia kupitisha bajeti hiyo aliwataka kuonesha mfano kuwa mstari wa mbele hasa katika mwaka huu ambao unaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na Rais katika kuwahamasisha wananchi kushiriki shuhuli mbalimbali za maendeleo ambazo zitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa manispaa  hiyo kusonga mbele na madiwani wote kurudi kwenye baraza hilo kwa mara nyingine.
Mhagama  ambaye  pia ni diwani wa kata ya Matogoro alisema kuwa kwa hivi sasa ni vyema kila diwani akajitahidi kumalizia viporo vya miradi mbalimbali vya maendeleo kwa wananchi
wake ili waweze kuwa na imani nae na kumchaguwa tena kuwa diwani kwa  mara nyingine.
 MWISHO.




Chapisha Maoni

 
Top