0
Mgombea Ubunge Jimbo la Songea Mjini kwa tiketi ya CCM Leonidas Gama akizungumza jambo na Waandishi wa Habari

 Mgombea Urais DKT MAGUFURI akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Songea Mjini kwa tiketi ya CCM Leonidas Gama
 
NA STEPHANO MANGO, SONGEA


ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye kwa sasa anagombea Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Songea Mjini Leonidas Gama amewaomba wananchi wa songea waone umuhimu wa kumpa kura mgombea urahisi kwa tiketi ya ccm Dr. John Pombe Magufuli kwa kuwa ni mtendaji kazi mzuri na ni mwadirifu.


 Gama ameyasema hayo juzi kwenye uwanja wa Majimaji ambako umati mkubwa wa wakazi wa maeneo mbalimbali ya manispaa ya songea walihudhuria  kwenye mkutano wa kampeni wakati akijinadi mgombea Urais, Ubungea na madiwani wa chama hicho.


Alisema kuwa Dr. Mgufuli ni tingatinga ambalo limekuwa likifanya kazi kwa muda wote kwa lengo la kuleta manufaa makubwa kwa watanzania wote hivyo anastahili kwa kiasi kikubwa kuwa Rais ya Jamhuru ya Muungano wa Tanzania na si vinginevyo.


Gama pia amewaomba wakazi wa manispaa songea kuona umuhimu wa kumchagua ili awe mbunge wao kwa kuwa anatambua fika matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi  ambao wengi wao ni wakulima na wafanyabiashara.


Alisema kuwa songea inachangamoto nyingi zinazotakiwa zifanyiwe kazi na mwakilishi mzuri kwenye bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo yeye ni greda lenye uwezo wa kusawazisha changamoto zote zilizopo ambazo wagombea wengine.


Mapema mgombea urahisi Dr. Magufuli ambaye kwa muda wote wanashangiliwa na umati mkubwa wa watu waliofika kumsikiliza wakati akijinadi alisema kuwa mkusanyiko mkubwa uliojitokeza  songea mjini ni wanasiasa wa vyama vyote hivyo endapo atapewa ridhaa ya kuwa Rais atakuwa ni kiongozi mwenye kuwajali watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama.


Dr. Magufuli alisema kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa rais wa nchi serikali yake haitaweza kuruhusu wakulima wakopwe mazao yao bali itahakikisha wakulima wanatafutiwa masoko ya mazao yao ya uhakika na kwamba kiongozi yeyote atayekwenda tofauti na maagizo yake atamuajibisha.


MWISHO


Chapisha Maoni

 
Top