KAMANDA WA POLISI RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
NA STEPHANO MANGO.SONGEA
JESHI
la Polisi Mkoani Ruvuma Linamtafuta Edwin Mrope (39) mkazi wa Lizaboni manispaa
ya songea kwa tuhuma za kumpiga mtoto wake kichwani wa umri wa mwaka 1 na
kumsababishia kifo wakati walipokuwa anamshushia kipigo mke wake aliyekuwa
amembeba mtoto huyo mgongoni aliyetambulika kwa jina la Wapekee Mrope (1).
Akizungumza
na mtandao huu jana mchana ofisini kwake kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo
msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 12 jioni huko
katika eneo la Lizaboni manispaa ya songea.
Kamanda
Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea wakati Mrope alipokuwa anagombana na
mke wake Lucy Lupogo ambaye inadaiwa alishushiwa kipigo sehemu mbalimbali za
mwili huku akiwa amembeba mtoto wake mgongoni na kisha alimvuta mkono wa kulia
na kumsababishia uvimbe mkubwa kwenye mkono huo.
Alifafanua
zaidi kuwa inaadaiwa wakati Lupogo anapigwa na mume wake huku akiwa amembeba
mtoto Wapekee ghafla mtoto huyo alipigwa kichwani na fimbo na kumsababishia
maumivu makali jambo ambalo lilisababisha wamkimbize hospitali ya mkoa kwa
matibabu zaidi ambako baada ya kupokelewa mda mfupi tu alifariki dunia
Alisema
kuwa uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa chanzo cha ugomvi ni kwamba Mrope
alikuwa anadaiwa fedha alizokuwa amekabidhiwa na mke wake ili akamunulie vifaa
vya ndani vya nyumba yao jambo ambalo lilileta mzozo wakati aliposhindwa
kurejesha fedha au vifaa alivyoagizwa akanunue.
Alieleza
zaidi kuwa uchunguzi huo umebaini
kuwa fedha hiyo mke wake aliyekuwa
anamdai mume wake alikuwa ameipata baada ya kuuza ufuta lakini mrope fedha hiyo
alikuwa tayari ameshaitumia kwa starehe zake na kwamba kwa sasa hivi polisi
inaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo ambaye inadaiwa amekimbia kwenda mpakani mwa
msumbiji na Tanzania lakini jitihada zinafanywa za kuhakikisha kuwa
a
nakamatwa.
MWISHO
Chapisha Maoni