NA STEPHANO MANGO,SONGEA
SIKU TATU kupita baada ya ajali ya Lori lililosheheni makaa ya mawe kutokea katika kijiji cha Gumbilo wilayani songea na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi wawili ajali nyingine jana huko katika kijiji cha makwaya wilayani songea na kusababisha mtu mmoja kufa papo hapo na kujeruhi watu wawili baada ya gari hiyo kushindwa kapanda mlima kisha kuanza kurudi nyuma na kupinduka.
Akizungumza na MTANDAO HUU jana mchana ofisini kwake Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi alisema kuwa tukio hilo lilitokea septemba 15 majira ya saa 6 mchana huko katika kijiji cha makwaya kwenye barabara ya kutoka songea kwenda kijiji cha muhukuru mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Alimtaja aliyekufa kuwa ni Yakobo Nyongolo (24) mkazi wa songea Mjini na majeruhi wa ajali hiyo wametajwa ni Mussa garahenga (32) mkazi wa kihesa manispaa ya Iringa na Dunia Machota Maginga mkazi wa kijiji cha kibara kilichopo wilayani Bunda mkoa wa Mara.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio gari lenye namba za usajiri T480 BVU aina Jiefang ambalo lilikuwa linatoka songea mjini kwenda muhukulu ambalo lilikuwa linaendeshwa na Juma Gassa (28) mkazi wa eneo la Luhila manispaa ya Songea lilishindwa kupanda mlima na baadaye lilianza kurudi nyuma kisha lilipinduka na kusababisha kifo cha Nyongolo na majeruhi wawili ambao walikimbizwa hospitali ya serikali ya mkoa songea kwa matibabu na jana mcha wameruhusiwa kurudi majumbani mwao.
Kaimu kamanda Malimi alisema kuwa kwa hivi sasa Jeshi la polisi mkoani humo linamsaka dereva wa gari hilo Juma Gassa ambaye inadaiwa alikimbikia na kutokomea kusiko julikana mara tu baada ya ajali hiyo kutokea na chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa licha ya kuwa taarifa za awali zimedai kuwa gari hiyo ilishindwa kupanda mlima baadaye lilianza kurudi nyuma kisha kupinduka.
MWISHO
Chapisha Maoni