![]() |
Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa |
![]() |
Wazee wakifuatilia moja ya mikutano ya kujadili changamoto zinazowakabili |
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
WAZEE wa Halmashauri ya
Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamemtaka mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu ujao
kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi kwa awamu ya tano amalize kero zinazowakabili ambazo zimetungiwa sera lakini hazitekelezwi
Wito huo umetolewa jana
na Mwenyekiti wa Baraza huru la wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Salum
Mwale wakati akichangia mada kuhusu
mahitaji na matarajio ya wazee wa Tanzania iliyoandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali linalowahudumia wazee Nchini (PADI) lenye makao makuu mjini Songea kwenye
mkutano uliowakutanisha wazee na waandishi wa habari.
Mwale alisema kuwa
wazee kwa muda mrefu wamelitumikia Taifa la Tanzania katika sekta mbalimbali
zilizo rasmi na zisizo rasmi na wamekuwa chimbuko kubwa na mhimili wa taifa la Tanzania
wamekuwa wakitoa jasho jingi katika kuhakikisha kuwa taifa linasonga mbele
lakini bado wanaendelea kutoa mchango wao kwa kujinyima sana hasa ikizingatiwa
hali zao za kiuchumi ni mbaya sana.
Alisema kuwa ili
kuhakikisha vijana wanapata elimu na maisha bora kwa lengo la kuboresha uchumi
wa nchi kwa kizazi kijacho bado wazee wanaendelea kuuumia na Serikali
haionyeshi kuwasaidia kwa kuwapa
pensheni.
Hivyo amemuomba Rais
ajaye wa Serikali ya awamu ya tano kazi kubwa ya kwanza atayoanza kuifaanya ni
vyema aangalie namna ya kuwasaidia wazee kwa kuhakikisha kuwa wanapatiwa
pensheni ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa baadhi ya changaamoto
wanazokabiliana nazo.
Kwenye mkutano huo
uliofanyika kwenye kituo cha kulelea wazee kilichopo eneo la Unangwa nje kidogo ya Manispaa ya Songea Edita Nchimbi
ambaye ni mjumbe wa Baraza huru la wazee wa Manispaa ya Songea alisema kuwa pensheni
kwa wazee ni muhimu sana hivyo ni vyema Serikali ijayo ikachukua jukumu la
kuwatambua wazee wote hapa nchini kwa
kuwapa huduma mbalimbali zikiwemo za matibabu kwenye zahanati, vituo vya afya
na hospitali za serikali.
Kwa upande wake Daud
Mpangala ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la wazee ameiomba serikali ya wamu ya
tano itakapoanza kufanya kazi isikilize kilio cha wazee wanaohitaji kusaidiwa
kupatiwa pensheni na huduma zingine tofauti na ilivyo sasa wazee wamekuwa
wakikabiliana na changamoto nyingi kwa vile hawana uwezo kiuchumi.
MWISHO
Chapisha Maoni