Mkuregenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Sixberth Valentini
Kaijage
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MGOMBEA Ubunge jimbo la peramiho wilaya ya
songea kupitia chama cha mapinduzi(ccm) Jenister Mhagama ameweka pingamizi la
uteuzi la mgombea ubunge wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika
jimbo hilo Erasmo Mwingira ambaye katika fomu yake imeonyeshwa kuwahaina muhuri
wa mahakama na fomu yake haionyeshi kuwa amehapa kwa mahakama gani.
Akizungumza na Mtandao huu jana ofisini
kwake msimamizi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wa jimbo la Peramiho ambaye pia ni
mkuregenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya songea Sixberth Valentini
Kaijage alisema kuwa pingamizi hilo
limetolewa jana na mgombea Mhagama baada ya kugundua kuwa kwenye fomu ya mgombea
mwingira ina kasoro.
Alifafanua zaidi kuwa mchakato wa uteuzi
wa wagombea ulianza rasmi Agost 8 mwaka huu na siku ya mwisho ya kuwasilisha
ilikuwa ni Agosti 21 mwaka huu ambapo kwa jimbo la peramiho kilikuwa na
wagombea watatu toka chama cha mapinduzi (ccm) mgombea wake alikuwa ni Jenister
Mhagama, Chadema ni Erasmo Mwingira na Democratic party (DP) ni Claudis Haule
Claudis.
Alisema kuwa siku ya uteuzi walioteuliwa
ni wagombea wawili ambao ni Jenister mhagama wa chama cha mapinduzi (ccm) na
Claudis Haule Claudis wa chama cha demokrasia na maendeleo na fomu majina ya wagombea zilibandikwa kwenye mbao za
matangazo lakini mgombea wa ccm jenister alimuwekea pingamizi mwenzake mgombea
wa chadema Mwingira ambalo lilipokelewa na msimamizi wa uchaguzi Agost 22 mwaka
huu.
Alisema baada ya kupokelewa pingamizi
hilo msimamizi wa tume ya uchaguzi ya Taifa jimbo la Peramiho alimjulisha
mgombea wa Chadema Mwingira juu ya
pingamizi hilo ili apate nafasi ya kutoa ufafanuzi au maelezo ya pingamizi
lilitolewa ndani ya masaa 24.
Alisema katika fomu hiyo iliyowekwa pingamizi
mhuri uliowekwa na mahakama sio ule ambao ulikuwa unahitajika na tume ya Taifa
ya uchaguzi pia katika fomu yake mgombea Mwingira
imeandikwa halmashauri ya songea kuweka pingamizi amedai kuwa mgombea
mwingira hajaonyesha uhalisia wa
halmashauri anayogombea.
Hata hivyo Mwingira amesema kuwa yeye aliomba kugombea nafasi ya
ubunge kwenye jimbo la peramiho ambalo lipo kwenye halmashauri ya wilaya songea
na mhuri ulitumika kwenye fomu yake ni wa mahakama na
Chapisha Maoni