Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bw. Mtani akikabidhi baiskeli kwa Mgani Kazi wa kijiji cha Mtonya Bi. Zingua Moyo
Kaimu Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bw. Mtani (Mwenye Suti)akikabidhi baiskeli kwa Magani Kazi wa kijiji cha Mtonya Bi. Zingua Moyo,katika mwenye shati la mikono mirefu lenye langi ya bluu ni Afisa Ugani wa Taasisi ya ACTN Abiud Gamba
Bw. Saidi Chalamanda akiwa amepanda baiskeli aliyokabidhiwa kama Mgani kazi,wa kwanza kuliamwenye shati la mikono mirefu lenye langi ya bluu ni Afisa Ugani wa Taasisi ya ACTN Abiud Gamba
Kaimu Mkurugenzi Bi. Wenseria Swai akikabidhi moja ya baiskeli kwa wagani kazi 13 kwa niaba ya wenzao,wa kwanza kulia ni Afisa Ugani kutoka taasisi ya Mtandao wa Kilimo Hifadhi Afrika (ACTN) , Abiud Gamba
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MAAFISA ugani wametakiwa kufanya
kazi zao kikamilifu ili kuweza kuwasaidia wakulima kupata elimu bora ya kilimo
ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao yao ya kiuchumi na kibiashara nchini
Wito huo umetolewa jana kwenye
Viunga vya Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Songea na Afisa Ugani wa Taasisi ya
African Conservation Tillage Network, ACTN Abiud Gamba wakati wa tafrija fupi ya
kukabidhi baiskeli kwa wakulima wa wilaya ya Namtumbo na Songea Vijijini
Gamba alisema kuwa maafisa ugani
ni nguzo muhimu sana ya kukuza kilimo na kukifanya kiwe mkombozi mkubwa kwa
wakulima na taifa kiujumla hivyo ni vyema maafisa hao wakaacha tabia ya kukaa
maofisini na badala yake waende kwa wakulima na vikundi vyao kwenda kuwaelekeza
kanuni bora za kilimo
Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu
wa kilimo nchini ACTN kwa kushirikiana na washirika wake katika mradi wa
Kuongeza Tija ya Uzalishaji nyanda za juu kusini mwa Tanzania (Integrated Bead
Basket Project) wametoa baiskeli 25 kwa wakulima wa wilaya za Namtumbo na
Songea vijijni ambao ni watoa huduma ya kuwawezesha wakulima wenzao maarufu
kama wagani kazi katika elimu ya kilimo hifadhi
Alifafanua kuwa baiskeli hizo
zitawasaidia kutafuta masoko, kuvitembeleavikundi vya wakulima, kutafuta
pembejeo za kilimo na kutembeleana na kupeana elimu ya fedha katika vijiji
vyao.
“Hii ni kuwawezesha wagani kazi
hao waliojengewa uwezo na Taasisi hiyo ya ACTN kutoa elimu ya ugani na ushauri
wa masuala ya kilimo katika jamii zao kwa kushirikiana na maafisa ugani wa
vijiji husika” alisema Gamba
Alifafanua kuwa kwa Songea vijiji ambavyo
vimenufaika na mradi huo ni Namatuhi, Mpitimbi, Litapwasi, Matimila, Gumbiro,
Ngadinda, Mkongotema, Madaba na Lilondo na Kwa Namtumbo ni vijiji vya Kitanda,
Naikesi, Luhimbalilo, Mtonya, Rwinga, Mandepwende, Namanguli, Litola na
Mchomoro.
Alieleza kuwa baadhi ya majukumu
yanayofanywa na Taasisi hiyo ya ACTN ni pamoja na kufanya tafiti za udongo ambo
tayari sampuli za udongo zimeshachukuliwa kwenye vijiji hivyo kwa ajili ya
utafiti kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa Kilimo ya Uyole – Mbeya,
Mafunzo ya Kilimo Hifadhi kwa
wagani kazi na wakulima, kuazisha mashamba darasa ya kilimo hifadhi na
urutubishaji husishi wa udongo, mafunzo kwa vitendo kupitia matukio mbalimbali
kamavile Nanenane, siku za wakulima na mambo mengine
Akitoa shukrani kwa niaba ya
wakulima wenzake Emmanuel Mango kutoka kijiji cha Kitanda Wilaya ya Namtumbo
alisema kuwa baiskeri hizo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia wakulima
katika mambo mbalimbali kwenye maeneo yao
Mango alisema kuwa wadau hao
wanatakiwa waisaidie jamii kubwa kwa kuwapa maafisa ugani pikipiki badala ya
baiskeli kwani maeneo mengi jiografia yake imekaa vibaya kutokana na kuwa na
milima na kuifanya baiskeli kutokuwa nyenzo sahihi ya usafiri kutokana na
matumizi mabaya ya muda
Akizungumza kwenye hafla hiyo Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Wenseria Swai aliwashukuru wadau
wa kilimo hifadhi kwa kazi zao nzuri wanazozifanya na kuwafikia wakulima
Swai alisema kuwa Serikali
inatambua wadau hao katika kukuza kilimo bora kwa maendeleo ya wananchi na
taifa kwa ujumla wake na kwamba serikali itaendelea kuthamini na kuenzi mchango
huo muhimu kwa uchumi wa taifa
MWISHO
MWISHO
Chapisha Maoni