0


                                   Charles Mhagama

NA STEPHANO MANGO,SONGEA
ALIYEKUWA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Charles Mhagama katika kipindi kilichopita ameshindwa kutetea kiti chake cha udiwani wa Kata ya Matogoro kupitia chama cha Mapinduzi baada ya Mgombea udiwani wa Kata hiyo kupitia chama cha wananchi Cuf Alawi Kawelea kuibuka mshindi

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Songea Mjini Rafael Kimari alisema kuwa chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kushinda kata 16 na chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda kata 4 na chama cha wananchi Cuf kimeshinda kata 1 na kwamba jimbo lote lina kata 21

Kimari aliwataja washindi wa Ccm na kata zao kwenye mabano, Oddo Mbunda(Mjimwema), Festo Mlelwa(Seedfarm) Mshawej Hassan(Subira) Maurus Lungu(Mletele) Yobo Mapunda(Lilambo), Lotari Mbawala(Mshangano) Cresensia Kapinga(Ndilimalitembo)na Osmund Kapinga(Mwengemshindo)

Aliwataja wengine kuwa ni Wilbart Mahundi(Ruhuwiko), Ismail Aziz(Misufini),Shaib Kitete(Mjini),Hussen Abukadi(Majengo),George Oddo(Lizaboni),Golden Sanga(Bombambili),Izack Lutengano(Msamala) na Mussa Mwakaja(Mateka)

Msimamizi huyo alizitaja kata ambazo Chadema  imeshinda ni Rashid Msuso(Ruvuma),Mussa Ndomba(Tanga) Martine Mlata(Matarawe)Seneta Yatembo(Mfaranyaki) na Alawi Kawelea (Matogoro) ambaye ameshinda kiti hicho kupitia chama cha wananchi Cuf

Alisema kuwa mpaka sasa hajapokea malalamiko yoyote kuhusiana na matokeo hayo na kwamba hali hiyo inaonyesha kuwa tume ya uchaguzi imetenda haki yake vizuri na wananchi wametumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua kiongozi ambaye wanamtaka
MWISHO








Chapisha Maoni

 
Top