NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WASHAURI
14 wa mahakama za mwanzo za Mfaranyaki na songea mjini katika Halmashauri ya
Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamegoma kufanya kazi hiyo baada ya kutolipwa
posho kwa miezi mitano.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutotajwa majina yao washauri hao
waliiyambia TANZANIA DAIMA kuwa tangu mwezi mei mwaka huu hadi sasa hawajapata posho
za vikao vya mahakama na wamejaribu kwa muda mrefu wapatiwe posho zao lakini
hamna mafanikio.
Walisema
kuwa kutokana na hali hiyo wamelazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kugoma tangu
oktoba 15 mwaka huu na kwamaba hivi sasa wapo majumbani mwao wakisubiri uongozi
wa mahakama utachakua hatua gani.
Walifafanua
zaidi kuwa walikuwa wakiingia gharama kubwa ya nauli ya kutoka majumbani kwao
kwenda mahakamani kwa ajili ya kwenda mahakamani kusikiliza kesi mbalimbali
lakini posho za vikao vyao wameshindwa kuzipata hivyo wameiyomba serikali
kupitia idara ya mahakama kuona umuhimu wa kuwatambua washauri wa mahakama
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha posho zao kuzipata kwa wakati.
Mwenyekiti
wa washauri ya mahakama ya mwanzo ya Songea mjini Dominick Njelekela
alipohojiwa na TANZANIA DAIMA mwishoni mwa wiki kuhusiana na mgomo alisema kuwa
wameamua kwa pamojaa kuto endelea kwenda mahakamani kufanya mambo ya ushauri na
badala yake wakisubiri mahakama kama itawalipa posho zao za miezi mitano ilizopita.
Njelekela
alisema kuwa Mahakama ya mwanzo ya songea mjini inawawashauri wa mahakama 8 na
katika mahakama ya mwanzo ya mfaranyaki kunawashauri sita ambao wote kwa pamoja
wameamua kugoma mpaka walipwe posho zao.
Hata
hivyo hakimu Mfawidhi wa mahakama ya mwanzo ya songea mjini Catherine Mattaka
alipohojiwa na TANZANIA DAIMA mwishoni mwa wiki ofisini kwake alizibitisha kuwa washauri
nane wa mahakama hiyo wamegoma kufanya kazi wakidai kuwa hawajalipwa posho zao
lakini alikataa kutoa ufafanuzi zaidi kwa madai kuwa yeye sio msemaji.
Kwa
upande wake mtendaji mkuu wa mahakama kuu kanda ya songea Beatus Benedictusi
alipohojiwa na nipashe kwa njia ya simu kuhusiana na mgomo huo wa wawashauri wa
mahakama ya mwanzo alikataa kutoa ufafanuazi zaidi na baadaye alikata simu.
TANZANIA DAIMA haikukata tama ililazimika kumtafuta afisa mtumishi wa mahakama hiyo Brian
Haule kwa kumpigia simu yake ya kiganjani na kumtaka atoe ufafanuzi kusiana
mgomo wa washauri wa mahakama ya mwanzo ya mfaranyaki na songea mjini naye
alizibitisha kutokea mgomo lakini hakutaka kuendele kutoa ufafanuzi zaidi na
alidai kuwa atapga simu baada ya nusu saa ili aweze kunifafanulia zaidi lakini
hakufanya hivyo na baadaye TANZANIA DAIMA ilirudia tena kumpigia simu zaidi ya mara
mbili lakini haikupokelewa.
Mwisho.
Chapisha Maoni