0

NA STEPHANO MANGO,SONGEA
 
WAZEE wa Halmashauri ya manispaa ya songea Mkoa wa Ruvuma wamemtaka mgombea urasi katika uchaguzi mkuu ujao hatakayefanikiwa kushinda ni vyema aone umuhimu kwanza wa kuwakumbuka wazee ili waweze kupatiwa uduma mbalimbali ikiwemo pensheni itakayoweza kuwapunguzia makali ya maisha.
 
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi mtendaji mkuu wa shirika lisilo la kiserikali linalowahudumia wazee (PADI) lenye makao makuu mjini songea Isikaka Msingwa kwenye sherehe za maazimisho ya siku ya wazee duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya manispaa hiyo.
 
Alisema kuwa wakati idadi kubwa ya wazee inazidi kuongezeka hapa nchini bado wazee wanashindwa kupata huduma muhimu wanazopaswa kuzipata kama vile matibabu na mahitaji mengine.
 
Msigwa alieleza kuwa ipo aja kwa wazee kuwashirikisha kwenye vyombo mbalimbali vy amaamuzi ambapo alifafanua kuwa wazee wanapaswa kuwa na wawakilishi bungeni na maeneno mengine jambo ambalo endapo likifanikiwa wazee wataweza kusikilizwa kilio chao cha muda mrefu cha kutaka wazee wote hapa nchini wawe wanalipwa pensheni kama nchi nyingine ambazo zimeweza kufanikiwa.
 
Ameiyomba serikali ya awamu ya tano ya jamuhiri ya muungano wa Tanzania ihakikishe sheria inatungwa kwa lengo ya kuwahudumia wazee kwa kuwapatia pensheni wazee wote tofauti na ilivyo sasa pensheni inatolewa kwa wafanyakazi.
 
Kwa upande wake mgeni rasm katika maadhimisho hayo ya siku yaw zee duniani katibu tawala  wa mkoa wa Ruvuma Hasani Bembeyeko aliyewakilishwa na katibu tawala wa wilaya ya songea Juma Ally aliesma kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee ambao wamefanya kazi nyingi ikiwemo  ya wapiganaji ya kumtoa nduli Idd amini wa Uganda.
 
Alisema kuwa pia serikali itahakikisha wazee wote wanalindwa na kukemea kwa nguvu zote mauwaji ya vikongwe na amewaomba wazee wazidi kuiyombea amani nchi ya Tanzania na kwamba serikali tayari inayo sera ya wazee ambayo inaendelea kufanyiwa kazi wame na subira.
 
Mwisho.

Chapisha Maoni

 
Top