KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
JESHI LA
polisi Mkoani Ruvuma imepiga marufuku kwa mtu yeyote au makundi ya watu wa
kutoka vyama mbalimbali vya siasa wanaodaiwa kutaka kuandamana kushinikiza
kuteuliwa kwa matokeo ya uchaguzi ya ngazi mbalimbali za uongozi (UDIWANI,
UBUNGE NA URAIS) yaliyotangazwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
mkoani Ruvuma.
Akizungumza
na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Mihayo Msikhela
alifafanua zaidi kuwa taarifa za ktaka kufanya maandamano baadhi ya watu au
makundi toka kwenye vyama vya siasa jeshi la polisi tayari limezipata kupitia
vyanzo vya baadhi ya watu waaminifu.
Alisema
kufuatia taarifa hizo jeshi la polisi mkoani humo limetoa tahadhari kwa mtu,
kikundi cha watu walio na nia hiyo kuwa ni kosa kufanya maandamano yasiyokuwa
na kibali kwa mujibu wa kifungu cha 74 cha sheria ya mwenendo ya makoa ya
jinai.
Alifafanua
kuwa kifungu hicho kinakataza mikusanyiko isiyo halali na kufanya hivyo ni
kukiuka sheria hiyo hivyo ni marufuku kwa mtu yeyote au makundi ya aina yoyote
toka kwenye vyama vya siasa kufanya mikusanyiko au maandamano ambayo sai
halali.
Kamanda
Msikhela alisema kuwa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma imejipanga kikamilifu
kuzuia maandamano haayo na amewataka wananchi wa mkoa huo kutoshawishia
na mtu yoyote kuingia katika maandamano ambayo kimsingi yamelenga kuleta
vurugu na kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa wa Ruvuma.
Aidha
jeshi la Polisi mkoani humo limetoa wito kwa watu au vikundi vinavyoshawishiwa
na vyama vya siasa kuona namna ya kutafuta njia nyingine mbadala ya kupata
suruhisho kwa mujibu wa sheria hivyo kwa mtu yeyote atakayekutii sheria hiyo
atachukuliwa sheria staiki ikiwa ni pamoja na kukamatwa ana kufikishwa
mahakamani na si vinginevyo.
MWISHO.
Chapisha Maoni