0

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Ruvuma(TAKUKURU) inamshikiria na kumuhoji Mkaguzi wa mahesabu wa ndani wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Philimon Lenard kwa kuhisiwa kuhusika na vitendo vya rushwa

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma Yustina Chagaka alisema kuwa Philimon Lenard alikamatwa machi 4 mwaka huu baada ya ofisi yake kupekea taarifa kutoka  kwenye vyanzo mbalimbali kuhusiana na masuala ya rushwa aliyokuwa anayafanya

Chagaka alisema kuwa toka machi 4 mpaka leo bado anashikiria,anahojiwa na kupekuliwa ili kuweza kubaini ukweli wa taarifa ambazo tumezipokea kuhusu mwenendo wake wa kazi na masuala ya rushwa na tukikamilisha  na kama itabainika ukweli wa taarifa hizo hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa za kumfikisha mahakamani

“Kwasasa tunaendelea kumhoji na kumfanyia uchunguzi wa awali hivyo hatuwezi kuzitaja taarifa au malalamiko tuliyoyapokea na hatua tulizozichukua kwani kwa sasa ni mapema mno tukimaliza uchunguzi wetu basi mambo yote yatakuwa bayana kwasasa uchunguzi unaendelea” alisema Chagaka

Aidha Kamanda wa Takukuru Mkoani humo Yustina Chagaka aliwatoa wito kwa mwananchi yoyote kujitokeza kutoa taarifa zozote zinazohusiana na vya rushwa vinavyofanywa na mtu yoyote kwani kwa kufanya hivyo kutaiwezesha taasisi kufanya kazi yake kwa haraka na kukomesha vitendo hivyo haramu
MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top