OMARY MBALALE AKIWA KATIKA POZI TOFAUTI TOFAUTI
OMARY MBALALE KUSHOTO AKIWA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI STEPHANO MANGO
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
AMA kweli hujafa na ujaumbika ndivyo kwa binadamu yeyote anavyoweza kusema mara akikutana na kijana Omary Said Mbalale mwenye umri wa miaka 30 na mkazi wa kijiji cha Libango wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma
Kijana huyo Omary anasumbuliwa na homa ya kifafa cha muda mrefu ambacho kimempelekea kupata madhara makubwa usoni mwake (homa mpya) kwani kwa sasa uso wake umeharibika na kumfanya macho yawe wazi na pua nayo kuwa wazi
Akizungumza na gazeti hili jana Omary Said Mbalale alisema kuwa homa ya kifafa ilimwanzia mwaka 2009 na kuendelea na matibabu bila mafanikio kutokana na umaskini unaomkabili yeye na familia yake na jamii ambayo inamzunguka imeshindwa kumsaidia
Mbalale anasema kuwa homa hiyo ameendelea mpaka sasa bila kupatiwa matibabu stahiki na kwamba juni 3 mwaka 2015 familia yake ilikuwa imeenda shambani na kumwacha pekee yake nyumbani kutokana na homa hiyo
Anasema kuwa akiwa nyumbani aliachiwa chakula jikoni ili kiweze kumsaidia mara anapokabiliwa na njaa, basi ilipofika mchana alijisikia kuumwa njaa ndipo alipoamua kuingia jikoni ili apakue chakula na aweze kula
“Ghafla niliangukia kwenye jivu la moto jikoni na nilipoteza fahamu kwa muda mrefu mpaka ndugu zangu waliporudi kutoka shambani na kuniokoa kwa kunitoa jikoni na kunipa huduma ya kwanza kabla sijapelekwa kwenye kituo cha afya cha Wilaya ya Namtumbo kwa matibabu kabla hajahamishiwa kwenye Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Songea kwa ajiri ya matibabu zaidi”alisema Mbalale
Alisema kuwa alilazwa katika Hospital ya rufaa ya Songea kwa muda mrefu mpaka majeraha yaliyotokana na jivu la moto yalipopona na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa ajiri ya kujipanga kwenda katika hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ajiri ya matibabu mengine zaidi ya kifafa na kufanyia marekebisho ya uso
Alieleza kuwa yeye hawezi kufanya kazi itakayomuingizia kipato kutokana na homa yake ya kifafa na homa ya macho kutoka nje baada ya kuungua na moto na hata familia yake nayo ina maisha magumu sana na hivyo kumkosesha fursa ya kwenda katika hospital kubwa jijini dare s salaam kwa ajiri ya matibabu
Anasema kutokana na hali hiyo aliamua kutoka wilayani Namtumbo na kuja Mjini Songea ambako yalipo makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma ili aweze kupata msaada kutoka kwa wasamalia wema, taasisi mbalimbali ili aweze kufanikisha matibabu ya maradhi yanayomsumbua
“Nilifanikiwa kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya songea na kufanikiwa kupata kibali januari 29 mwaka huu cha kuomba wasamalia wema na taasisi michango yao ya hali na mali chenye Kumb.Na.AB.308/398/01/176. Ili niweze kutibiwa homa ya kifafa,macho kutoka nje kutokana na kukosa nyusi na ngozi ambayo inashikiria jicho, pua kuwa wazi” alisema mbalale
Alisema kuwa yeyote anayeguswa na homa hiyo anaweza kumchangia kupitia Mpesa 0755-335051 au Tigopesa 0715-335051 kwani kwa sasa anateseka sana kwakupita mitaani kuomba michango na amekuwa akipata fedha kidogo ambazo amekuwa akila na nyingine kununulia dawa kutokana na maradhi anayoyapata ya kulala nje na vumbi zinazomuingia puani na machoni
Kijana huyo alibahatika kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi Libango iliyopo wilaya ya Namtumbo mwaka 1999 akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto 6 wa mzee Said Mbalale Kulasa anatamani kuwa na mke lakini wanawake wamekuwa wakimkimbia kutokana na malazi hayo
MWISHO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni