WAENDESHA BODA BODA 20 MBARONI KWA KUVUNJA GARI LA MWANAJESHI
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikiria waendesha bodaboda 20 wa manispaa ya Songea ambao wanadaiwa walimshambulia askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ wa kikosi cha 411 KJ cha Ruhuwiko kilichopo mjini hapa na kulishambulia kwa kupiga mawe gari alilokuwa kiliendesha baada ya kumgonga mtembea kwa miguu.
Akizungumza jana na awaandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saatatu za usiku huko katika maeno ya shule ya Msingi mfaranyaki iliyopo karibu na kitu kikuu cha polisi songea mjini.
Alimtaja askari wa jeshi la wananchi aliyejuruhuwa vibaya kwa kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili na waendesha bodaboda kuwa ni Samweli Nginila (32) askari wa kikosi cha 411 KJ cha Ruhuwiko ambako kwa sasa hivi amelazwa katika hospitali ya serikali ya mkoa Songea (HOMSO) Kwa matibabu
zaidi.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Nginila alijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na kupoteza fahamu baada ya kushambuliwa na waendesha bodaboda na kuvunja vioo vya gari alilokuwa akiliendesha kwa kulipiga mawe.
Alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa siku hiyo kabla yake ajali ilitokea maeneo ya majengo ambako Nginila alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajiri T 967 DAE aina ya Nissan XTRAIL akitokea kwenye Bar ya Ramour na alipofika kwenye eneo la majengo Mwanamke mmoja Bahati Mbero wa majengo akiwa anakatisha ghafla barabarani na kusabisha ajari kutokea kutokana na dereva Nginira kushindwa kumkwepa na kupelekea bahati kupata majeraha kidogo.
Alieleza zaidi kuwa kufuatia hali hiyo madereva wa bodaboda waliokuwa karibu na eneo la tukio walikusanyika kwa lengo la kumshambulia dereva wa gari hiyo hali iliyomlazimu dereva wa gari hiyo kuwasha gari yake na kukimbia ili kuokoa maisha yake na baadaye madereva wa bodaboda walimkimbiza lakini dereva wa gari hiyo alipofika maeneo ya shule ya msingi mfaranyaki jitihada za kukimbia zilishindikana kwani moja ya matairi ya gari yake lilichomoka na baadaye madereva yebo walimzingira na kumshushia kipigo pamoja na abiria watatu aliokuwa amewabeba na gari kulipiga mawe.
Amewataja abiria waliopigwa kuwa ni Kaumbya Kateka (24)mkazi wa majengo, Joyce Edson (24) Mkazi wa Mpambalyoto, na Jackline Mwita (22) mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Peramiho wilaya ya songea Vijijini ambao walikimbizwa hospitalini ambako walitibiwa na kuruhusiwa.
Aidha kamanda Mwombeji alisema kuwa katika Vurugu baadhi ya vitu vimepotea ambavyo ni mali ya Nginila ambapo amevitaja kuwa ni Simu mbili za mkononi ambazo hazijatambulika ni za aina gani na thamani yake, pochi ambayo ilikuwa imehifadhi vitambulisho vya kazi, kupigia kura, kadi za ATM za Bank ya NMB na CRDB pamoja na fedha taslimu shilingi 120,000/ elfu.
Hata hivyo kamanda Mwombeji alisema kuwa msako kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wengine waliohusika na taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa
zinafanywa mara tu baada ya kukamilika.
MWISHO
Chapisha Maoni