Kamanda wa polisi mkoa wa
Ruvuma Zubery Mwombeji
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MTEMBEA kwa miguu mkazi wa kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma Bitnes Ngonyani (5) amegongwa na trekta ambalo lilikuwa limefungwa tela lililokuwa limebeba watu 17 ambao wamenusurika kifo baada ya tela la Trekta hilo kupinduka na kuwasababishia majeraha.
Akizungumza na gazeti hili jana mchana ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zubery Mwombeji alisema kuwa ajali hiyo imetokea juzi majira ya saa kumi jioni katika barabara ya kutoka kijiji cha Hanga kwenda kijiji cha Kitanda.
Alifafanua zaidi kuwa watu waliojeruhiwa walitajwa kuwa ni Yakini Ndogoro(29), Basiri Ngonyani(25), Costantine Ngonyani(25), Goodluck Komba (32), Ismail Ndogoro(50), Asili Mwangama(20), Erick Komba(20) na Sanifa Nyoni(18) wote wakazi wa kijiji cha kitanda ambao hali zao ni mbaya na walikimbizwa katika hospitali ya mkoa ambako walilazwa kwa matibabu zaidi na abiria wengine 9 walitibiwa katika zahanati ya kijiji cha kitanda na hali zao zinaendelea vizuri.
Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio trekta lenye namba za usajiri T535 CWL aina ya SONALIKA lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye jina lake halijafahamika mara moja huku likiwa na tela lake ambalo lilikuwa na abiria 17 lilimgonga mtembea kwa miguu Bitnes na kumsababishia majeraha katika mwili wake
Mwombeji alisema pia tela la trekta hilo baada ya kumgonga mtembea kwa miguu lilipinduka na kupelekea majeraha kwa watu wote waliokuwa wamepanda trekta hilo ambapo kati ya watu hao 17 watu 9 walitibiwa na kuruhusiwa katika zahanati ya kijiji cha kitanda ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja na wengine 8 wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kutokana na kupata majeraha makubwa kwenye miili yao.
Kamanda Mwombeji alisema kuwa kwa sasa hivi jeshi la polisi mkoani humo linamsaka dereva wa treka hilo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa kukimbia na kutokomea kusiko julikana mara tu baada ya ajali hiyo kutokea.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimesababishwa na uzembe wa dereva wa Treka hilo ambalo lilikuwa limefungwa tela lililokuwa limebeba abiria wengi kupita kiasi kimakosa kupelekea kutokea ajali hiyo ambapo alifafanua kuwa treka hilo lilikuwa linatoka kijiji cha hanga kwenda kijiji cha kitanda huku likiwa limewabeba abiria wanaodaiwa walikuwa wanatoka kwenye mashindano ya mpira wa miguu kati ya vijiji hivyo kati ya hanga na kitanda.
Hata hivyo kamanda Mwombeji alisema kuwa polisi pia inamsaka mmiliki wa Trekta hilo ili hatua dhidi yake zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuendelea kumsaka dereva.
MWISHO

Chapisha Maoni