0
NA STEPHANO MANGO,SONGEA

WATU wawili wamejeruhiwa vibaya akiwemo askari polisi wa kituo cha polisi cha Lituhi wilayani Nyasa baada ya gari walilokuwa wamepanda ambalo lilikuwa linasafirisha mitihani ya darasa la saba kufeli breki na kupinduka .

Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi alisema kuwa tukio hilo lilitokea septemba 9 mwaka majira ya saa 12 asubuhi huko kwenye barabara ya kutoka Darpori kwenda Tingi katika eneo la kijiji cha mtetema  wilayani Nyasa.

Alifafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio gari lenye namba za usajiri T204 ADC aina ya LAND ROVER 110 ambalo lilikuwa linaendeshwa na Fulko Ndunguru (29) mkazi wa kijiji cha Lifakara wilayani Mbinga liliwajeruhi watu wawili ambapo askari H319 PC Abdallah (25) wa kituo cha Polisi Lituhi na Askari Mgambo Bernad Chanda (50) mkazi wa kijiji cha Lituhi.

Alieleza zaidi kuwa gari hilo ambalo lilikuwa limesheheni mitihani  lilikuwa linasambaza mitihani ya darasa la saba kwenye shule za msingi zilizopo kwenye maeneo ya vijiji vilivyopo wilayani Nyasa liliacha njia na kupinduka na kusababisha majeruhi hao ambao kwa sasa hivi wamelazwa katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Nyasa iliyopo katika mji mdogo wa Mbambabay.

Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi Malimi alisema kuwa  chanzo cha ajali ni kufeli breki za gari hiyo na kwamba dereva wa gari Ndunguru anashikiliwa na polisi wakati uchunguzi zaidi wa ajali hiyo ukiwa unaendelea na kwamba ukikamilika aatafikishwa mahakamani shitaka linalomkabili.

MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top