0
 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi

Na Stephano Mango, Songea

WATU watano wamekufa papo hapo  na wengine wawili wamejeruhiwa vibaya na wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma baada ya gari walilikuwa wakisafilia huku likiwa limesheheni makaa ya mawe kuacha njia na kupinduka kwenye kona za majimaji barabara ya kutoka songea kwenda njombe katika kijij cha Gumbilo wilaya ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Revokatus Malimi alilitaja tukio hilo kuwa lilitokea September 12 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Gumbilo nje kidogo ya manispaa ya songea.

Aliwata walio poteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Jaffar Ally Hakimu (40) ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo, Sadali Ally ambaye haikuweza kutambulika umri wake mara mmoja mkazi wa mkoa wa Morogoro, Mwalimu Gilbert Mbilinyi (42) mkazi wa kijiji cha Mkongotema, Dickson Nyandindi (32) mkazi wa Mbinga na Mohamed Hald ambaye na umri wake haukutambulika mara moja wala kabila na hafaamiki ni mkazi wa wapi.

Malimi aliwataja majeruhi kuwa ni Mussa Muchungwa (40) mkazi wa kijiji cha mkongotema na Julius Haule (39) mkazi wa kijiji cha Njambe wilayani nyasa ambaye inadaiwa kuwa alipanda gari hiyo katika eneo la msamala kwa lengo la kwenda morogoro kuwasalimia ndugu zake.

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio gari yenye namba za usajili T 906 CTR aina ya IVECO ambalo lilikuwa na tela lake lenye namba za usajili T618 CSN mali ya kampuni ya Everlest inayofanya kazi ya kubeba makaa ya mawe toka kwenye mgodi wa makaa ya mawe uliopo Lwanda wilayani mbinga kwenda jijini Dar es salaam ambalo lilikuwa linaendeshwa na Jafar Ally Hakimu likiwa kwenye mwendo mkali liliacha njia na kupinduka kwenye mfereji uliopo kandokando hiyo na kusababisha vifo vya watu watato hapopapo na majeruhi wawili.

Kaimu kamanda Malimi alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao ulimsababishia dereva kumudu usikani wa gari yake kwenye kona kali za majimaji na kupelekea kuacha njia na kupinduka.

Naye mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya serikali ya mkoa wa Ruvuma Dr. Philis Nyimbi akiwa kwenye wodi namba 2 ya jinsia ya kiume aliwaambia waandishi wa habari kuwa jana majira ya saa 2 za usiku wamepokea maiti tano na majeru wawili wa ajali hiyo ambapo alifafanua kuwa Moses Muchungwa amejeruhiwa mkono wa kulia ambao unatakiwa ufanyiwe upasuaji na katika maeneo ya kiuno na mgongo anatakiwa afanyiwe uchunguzi wa kina kwakuwa unaonyesha mifupa miwili imevunyika, na Julius Haule amepata michubuko na amepooza mkono wake wa kushoto na mguu wa kulia sehemu ambayo inadaiwa kuwa alishiliwa na kifusi cha makaa yam awe.

Kwa upande wao majeruhi Muchungwa na Haule wamewaeleza waandishi wa habari  kuwa tangu walipopanda gari hilo eneo la msamala manispaa ya songea gari hiyo ilikuwa inaenda kwa mwendo kasi huku dereva na utingo wake walikuwa wanakunywa pombe aina ya bia jambo ambalo lilisababisha abilia wa gari hiyo walianza kuwalalamikia lakini abilia walijibiwa kuwa musiogope kufa ni jambo la kawaida

Mwisho.

Chapisha Maoni

 
Top