Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Revokatus Malimi akionyesha jambo
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MAJERUHI wawili wa ajari iliyosababisha vifo vya watano baada
ya gari walilikuwa wakisafilia huku likiwa limesheheni makaa ya mawe kuacha
njia na kupinduka kwenye kona za majimaji barabara ya kutoka songea kwenda
njombe katika kijiji cha Gumbilo wilaya ya Songea wameeleza kuwa chanzo cha
ajari hiyo ni ulevi wa kupindukia
Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika kwenye wodi
namba 2 ya majeruhi iliyopo kwenye Hospital ya Serikali ya Mkoa wa Songea
majeruhi hao wameeleza kuwa tangu walipopanda kwenye gari hiyo dereva Jaffar
Ally Hakimu (40)na utingo wake Sadali Ally ambaye haikuweza kutambulika umri wake
mara mmoja walikuwa wanakunywa pombe kwa
fujo jambo ambalo liliwafanya abiria waanze kuwalalamikia
Majeruhi Mussa Muchungwa (40) mkazi wa kijiji cha mkongotema
alisema kuwa alianza kumshukuru mungu
kwa kumuepusha na kifo katika ajari hiyo ambayo
yeye alikandamizwa na makaa ya mawe mpaka alipokuja kuokolewa na watu waliofika kwenye eneo la ajari hiyo
Muchungwa alisema kuwa akiwa Songea mjini juzi majira ya saa
9: mchana alianza kutafuta usafiri wa kurudi kijijini kwake Matimila na ilipofika
saa 11:14 alifanikiwa kupata usafiri wa lori lililosheheni makaa yam awe lakini
baada ya kuondoka tu Dereva na utingo wake waliendelea kunywa pombe huku gari
likiwa linaendelea na safari
Naye majeruhi Julius Haule (39) mkazi wa kijiji cha Njambe
wilayani nyasa alisema kuwa ni mungu tu
aliwasaidia kutoka wakiwa hai kwani mabonge ya makaa yam awe yaliwaangukia na
ndio hayo hayo ndio yaliowasababishia vifo
Haule alisema kuwa kwasasa hivi anasikia maumivu makubwa
kwenye mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na ameiomba Serikali iangalie namna
bora ya kukemea madereva wazembe na kuwachukulia hatua kali za kisheria
madereva walevi kwani wakati
wanawalalamikia walijibiwa kuwa nyie mmekuwa wageni wa vifo na kwamba kila mtu
atakufa ndipo alipoamua kuhama kutoka mbele na kurudi nyuma
Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya serikali ya mkoa wa
Ruvuma Dkt Philis Nyimbi alisema kuwa
hali za majeruhi hao bado sio nzuri na jitihada za madaktari zinaendelea ili
kuboresha afya zao na kwamba Moses Muchungwa amejeruhiwa mkono wa kulia ambao
unatakiwa ufanyiwe upasuaji na katika maeneo ya kiuno na mgongo anatakiwa
afanyiwe uchunguzi wa kina kwakuwa unaonyesha mifupa miwili imevunjika
Kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma
Revokatus Malimi alilitaja tukio hilo kuwa lilitokea September 12 mwaka huu
majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Gumbilo nje kidogo ya Manispaa ya Songea.
Malimi alisema kuwa siku hiyo ya tukio gari yenye namba za
usajili T 906 CTR aina ya IVECO ambalo lilikuwa na tela lake lenye namba za
usajili T618 CSN mali ya kampuni ya Everlest inayofanya kazi ya kubeba makaa ya
mawe toka Mbinga kwenye mgodi wa makaa ya mawe uliopo Lwanda wilayani kwenda
jijini Dar es salaam ambalo lilikuwa linaendeshwa na Jafar Ally Hakimu likiwa
kwenye mwendo mkali liliacha njia na kupinduka kwenye mfereji uliopo kandokando
mwa barabara hiyo na kusababisha vifo vya watu watano hapopapo na majeruhi
wawili
Kufuatia ajari hiyo Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Malimi
amewataka madereva wa vyombo vya moto kuona umuhimu wa kufuata kanuni na
taratibu za barabarani sambamba na kuchukua taadhari kwa watumiaji njia wengine ili kuepuka ajari za mara kwa
mara ambazo zinaghalimu maisha ya watu ambao hawana hatia
Chapisha Maoni