NA STEPHANO MANGO,SONGEA
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Shukrani
Mkingwa (21) Mkazi wa Mfaranyaki Manispaa ya Songea kwa kukutwa na begi lililosheheni bangi zenye uzito wa kilo 11
ambazo alikuwa akizizafirisha kuelekea mkoani Iringa
Akizungumza jana na Gazeti hili Ofisini kwake Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema limetokea Novemba 23 mwaka majira
ya saa 12:30 asubuhi huko katika eneo la Mshangano nje kidogo ya Manispaa ya Songea
Msikhela alifafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Askari
Polisi waliokuwa dolia walifanikiwa kumkamata Mkingwa akiwa na bangi ambayo
alikuwa amehifadhi kwenye begi tayari kuisafirisha kuelekea Iringa lakini kabla
hajaondoka Askari Polisi waliokuwa kwenye eneo hilo walimtilia mashaka pamoja
na mzigo aliokuwa ameubeba
Alisema kuwa baadae Askari Polisi walifanikiwa kumkamata na
kuanza kumpekua na kukuta bangi kwenye begi lake na alipohojiwa alieleza kuwa
anataka kuelekea Iringa na kwamba alikiri kuwa mzigo huo ni wa kwake na pia
alionyesha ushirikiano kwa Askari hao kwa kuwapeleka sehemu ambayo ilikuwa ni
ghara la kuhifadhi bangi ambayo huwa inasafirishwa maeneo mbalimbali nchini
Alieleza zaidi kuwa Askari Polisi walipofanikiwa kufika
kwenye eneo hilo walifanya upekuzi ambapo baada ya kukamilisha walifanikiwa
kukamata mifuko mitatu iliyosheni bangi inayokadiliwa kuwa na kilo 19
“Kufuatia tukio hilo mimi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma
natoa wito kwa wakulima , wauzaji na watumiaji wa bangi ambayo ni haramu kuacha
mara moja na badala yake wajishughulishe na biashara zingine ambayo ni ya
halali”alisema Msikhela
Alisema kuwa msako mkali unaendelea wa kuwatafuta waharifu
wengine wanaojihusisha na matumizi ya bangi pamoja na wafanyabiasha wa kuuza
bangi kwani wananchi wanapaswa kujua kuwa matumizi ya zao hilo yanapelekea
kuongezaka kwa matukio ya uharifu hapa nchini
MWISHO
Chapisha Maoni