NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WATU watano wa kazi wa Kijiji cha Mapipili kata ya
Kitumbalomo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamelazwa katika Hospitari ya Wilaya
ya Mbinga wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kunywa togwa inayosadikiwa
kuwa na sumu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema
kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6 mchana huko katika kijiji cha
mapipili ambapo aliwataja waathilika wa togwa kuwa ni Edah Kapinga(25), Adelina
Nchimbi(23)
Wengine ni Paulina Komba(21) Stamili Mapunda(21) na mtoto
mdogo Stella Komba mwenye umri wa mwaka mmoja wote wakazi wa Kijiji hicho ambao
bado wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospital hiyo ya Wilaya
Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo inadaiwa awali watu hao
walikuwa wanakikundi kidogo cha ushirika cha kusaidiana kulima mashamba kwa
zamu kwa kila mwanakikundi na siku hiyo ya tukio inadaiwa wanakikundi
walialikwa na Edah Kapinga ambaye ni Mlemavu wa ngozi(albino) kwa ajiri ya
kumlimia shamba lake kama taratibu za kikundi hicho kilivyojiwekea
Alifafanua kuwa baada
ya kumaliza kulima shamba hilo Edah alikuwa amewaandalia wenzake kinyaji
cha aina ya togwa kama shukrani kwa kumlimia shamba na baada ya kumaliza kunywa
kinyaji hicho matumbo yao yalianza kuuma na kukimbizwa hospital ya Wilaya kwa
ajiri ya matibabu
Alieleza zaidi kuwa kufuatia uchunguzi wa Mganga aliyekwenda
eneo la tukio na kuchukua sampuli ya kinywaji hicho inaonyesha kuwa nafaka
iliyotumika kutengenezewa togwa hiyo hiyo ilikuwa na sumu ya kuulia wadudu
waharibifu wa nafaka
Alisema kuwa kabla ya kutengenezwa togwa hiyo nafaka
haikusafishwa kikamilifu hivyo amewataka wananchi wote wakiwemo wakulima
kuchukua taadhari kabla ya kupika vinywaji vya kienyeji ili kuepuka madhara
yatokanayo na sumu inayowekwa kwenye nafaka
MWISHO
Chapisha Maoni