Na, Stephano Mango, Songea
UCHAGUZI
wa kura za maoni nafasi ya ubunge na madiwani
wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma umemalizika kwa matokeo ya awali,
mkuu wa mkoa wa Kirimanjaro Leonidas Gama amewabwaga makada wenzake 7 kwa
kupata kura 6287 wakati aliyekuwa waziri wa mazingira Dokta Thereza Uviza
amepata kura 5600.
Katibu
wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Songe mjini Juma Mpeli akizungumza na
waandishi wa habari jana asubuhi ofisini kwake aliwataja makada wengine
waliokuwa wanawania nafasi hiyo ambao kura zao hazikutosha kuwa ni meneja
mwandamizi wa mitandao wa benki ya biashara ya China iliyopo jijini
Dar-es-salaam Mussa Gama mtoto wa marehemu Dk Raulence Gama alipata kura
1278,wengine ni katibu wa CCM wa wilaya ya Namtumbo Azizi Mohamedi Fakiri
alipata kura 1101,Erick Mapunda mhadhiri wa chuo kikuu cha sayansi na
teknorojia Mbeya alipata kura 908.
Mpeli
aliwataja wengine kuwa meneja masoko wa Claus FM Radio na TV ya jijini
Dar-es-salaam Raymond Mhenga amepata
kura 576 wakati mkuu wa wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara Francis Miti alipata
kura 475 na mwanasheria wakiri wa kujitegemea manispaa ya Songea Sebastian
Waliyuba alipata kura 265.
Alifafanua
zaidi kuwa wilaya ya Songea mjini inawanachama waliojiandikisha kwenye kitabu
cha orodha ya wanachama wa CCM ni 34,800 lakini wanachama waliojitokeza kupiga
kura za maoni ni 17,226.
Wakati
huohuo katika kituo cha kupigia kura eneo la Mwembechai kata ya Matarawe vilijitokeza vituko vilivyoonekana sio vya kawaida ambavyo
vinasadikiwa kuwa ni vya ushirikina
ambapo madawa yanayodaiwa kuwa ya kienyeji yalionekana yamemwagwa chini ya mlango wa chumba cha kupigia kura na radi
ilipiga majira ya saa za mchana huku jua kali likiwa linawaka na kusababisha
tafrani kubwa kwa wapiga kura.
Mmoja
kati ya mashuhuda wa tukio hilo Jafari Nindi(Ukuta) amesema kuwa majira ya saa
11 arfajiri katika kituo hicho wapiga kura waliowahi walikuta dawa ya mitishamba imemwagwa katika
mlango wa chumba cha kupigia kura.
MWISHO
Chapisha Maoni