MBUNGE MTARAJIWA WA JIMBO LA PERAMIHO JENISTA MHAGAMA AKIFURAHI BAADA YA KUPITA BILA KUPINGWA
Na Stephano Mango,Songea
WAZIRI wa sera na uratibu wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jenista Mhagama amepita bila kupingwa kwa sasabu wakati wa mchakato wa
kuchukua fomu za kuomba uongozi ndani ya chama wagombea wenzake wawili
waliojitokeza kuwania nafasi hiyo mmoja fomu ilisahiniwa na mtu mwingine ambaye
si mgombea na mwingine siku moja kabla ya kuanza kampeni alianguka ghafla
chooni wakati akijisaidia.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katibu
chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea Vijijini Rajab Huonde aliwataja wagombea
ambao walishindwa kuingilia kwenye kinyanganyiri hicho kuwa ni Lazaro Komba
Bunungu mfanyakazi wa Tanroads mkoa wa Tanga , pamoja na Clement Makaburi
Mwinuka mkazi wa Magagula .
Alifafanua kuwa, sababu zilizomfanya bunungu kushindwa
kugombea nafasi hiyo ni kwamba baada ya kupata ajali hiyo hakuweza kuleta
taarifa yoyote juu ya maendeleo ya ugonjwa wake hadi kampeni zilipokwisha ,na
mwinuka fomu yake ya kuomba uongozi ndani ya chama haikusainiwa na mgombea
mwenyewe.
Alisema kuwa jimbo la peramiho ambalo linakata 17 wanachama
wameridhia kumpitisha Jenista Mhagama kutokana na wagombea wengine kutoonekana
siku ya uchaguzi .
Wakati huo huo Mkurugenzi shirika lisilo la kiserikali
RUCCODIA Joseph Mhagama amewabwaga makada wenzake nane baada ya kupata kura
5081 ,akifatiwa na profesa Elieuther Mwageni
makamu mkuu wa chuo cha Ardhi wa fedha na utawala jijini Dar es salaam
aliyepata kura 993, wengine ni Mkuu wa wilaya ya Tarime Glolius Luoga (838),
mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya uhamiaji nchini Kinemo kihanamo (734),mkuu
wa shule ya sekondari ya kutwa London manispaa ya Songea Christopher Mwageni
(200) Limo Mwageni mwalimu shule ya
sekondari mpanda (84)
Huonde alifafanua kuwa, wagombea wengine wawili ambao ni
Tasilo Mahuwi na Venance Mgaya siku ya mwisho waliamua kujitoa kwa sababu
ambazo hawakuziweka wazi wakati pius mwageni fomu yake ya kuomba uongozi
baadaye ilibainika kuwa haikusainiwa na mgombea mwenyewe hivyo ilimfanya akose
sifa ya kugombea nafasi hiyo.
Mwisho

Chapisha Maoni