0
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Wenselia Swai



Baadhi ya wakulima wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi

         Baadhi ya pembejeo za kilimo 

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,imeipongeza taasisi ya African Conservation Tillage Netwok(ACTN)kwa jitihada zake za utoaji wa elimu ya ugani na uzalishaji kupitia teknolojia ya kilimo hifadhi na urutubishaji udongo kwa wakulima wadogo wadogo wa kijiji cha Madaba kilichopo Wilayani humo.

Pongezi hizo zilitolewa jana na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Wenselia Swai,wakati alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wakulima ambapo kiwilaya yalifanyika katika kijiji cha Madaba Wilayani humo.

Wenselia alisema kuwa teknolojia hiyo mpya imefika wakati muafaka ambapo imeanza kuleta matumaini mapya kwa wakulima wadogo wadogo na halmashauri kwa ujumla baada ya kuanza kupata mafanikio ya ongezeko la uzalishaji wa mazao ya Mahindi,Soya,Maharage na Mpunga  ambapo alidai kuwa  eneo kubwa la Songea ardhi yake haina rutuba.

Hata hivyo kaimu mkurugenzi huyo amewataka wakulima hao kutumia mbolea ya asili lwenye mashamba yao kwa ajili ya kurutubisha ardhi na kuepuka madhara  yanayosababishwa na mbolea za kemikali.

Nae msimamizi wa mradi huo unaoshirikisha taasisi ya BRITEN,RUDI,ACTN na benki ya CRDB kupitia ufadhili wa shirika la kuleta mapinduzi ya kijani Barani Afrika(AGRA) Frank Muhando alisema kuwa lengo kubwa la shirika hilo ni kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima ili waweze kuongeza uzalishaji wa mazao na kuwaongezea kipato ambapo amedai kuwa mpaka sasa limeweza kuzifikia nchi 17 ikiwemo Tanzania.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima,baadhi ya wakulima hao walisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja toka mradi huo uanze wameweza kupata mafanikio katika kilimo cha zao la Mpunga,Soya,Mahindi na Maharage tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma kabla ya kupata elimu hiyo.

Kwa upande wake mratibu wa mradi wa taasisi ya ACTN Abiud Gamba,ambaye pia ni Ofisa ugani alisema kuwa wakulima 25 wa kijiji cha Madaba wamenufaika na elimu hiyo ya uzalishaji kupitia teknolojia ya kilimo hifadhi na urutubishaji husishi wa udongo ambapo amedai kuwa mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya Kilolo,Ludewa,Songea na Namtumbo na kufanya idadi ya wakulima wakionufaika na elimu hiyo kufikia 100.

MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top