NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amewataka wafanyabiashara mkoani humo kutafuta njia ya kuzimaliza kero kati yao na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) badala yakujichukulia sheria mkononi ya kufunga maduka nakusababisha kuwepo kero kubwa kwa wateja wao wakiwemo wakulima wanaotoka vijijini kuja kutafuta mahitaji.
Mwambungu aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa wafanyabiashara uliofanyika kwenye ukumbi wa parokia ya bombambili jimbo kuu la Songea la kanisa katoliki ambao uliudhuliwa na mamia ya wafanyabiashara akiwemo mwenyekiti wa jumuhiya ya wafanyabiashara Tanzania Johnson Minja.
Alisema kuwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na wafanyabiashara hawawezi kutenganishwa kwani mfanyabiashara anapofanya biashara zake anatakiwa kulipakodi ya serikali hivyo hakuna sababu ya haina yoyote ya kuwepo mvutano usiokuwa na tija.
Alifafanua zaidi kuwa hakuna jambo baya la kuwaadhibu watu wasio na makosa ambao wanahitaji kupata huduma kwa wafanyabiashara lakini huduma imekuwa ikishindwa kupatikana kufuatia wafanyabiashara kuacha kufunga maduka jambo ambalo linaonekana kuwa ni kero kwa wananchi hivyo amewataka waache tabia hiyo ya kufunga maduka.
Mwambungu aliwaambia wafanyabiashara kuwa kwa sasa hivi ni vyema wajenge mazingira ya kuwa na mahusiano mazuri kati yao na mamlaka yamapato (TRA) ili kuboresha mapato ya serikali ambayo yanahitaji kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
“Ndugu zangu msifunge maduka kwa sababu gharama yake ni kubwa sana kutokana na kufungwa maduka hayo mnawaadhibu wananchi wasio kuwa na makosa ambao bado wanahitaji kupata huduma kutoka kwenu ninyi wafanyabiashara” Alisema Mwambungu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuhiya ya wafanyabiashara Tanzania Taifa Johnson Minja alisema kuwa jumuhiya hiyo ni kiunganishi kati ya wafanyabishara na serikali hivyo amewataka wafanyabiashara kuona umuhimu wakujenga mazingira ya kuwa karibu na mamlaka ya mapato kwa kuhakikisha kuwa kodi za serikali zinalipwa na kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi hao wanatakiwa kufichuliwa.
Minja alisema kuwa Tanzania imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi hivyo wafanyabiashara ni vyema waonyeshe mshikamano mkubw wa kuhakikisha kuwa biashara wanazozifanya inapaswa zilipiwe kodi.
Naye Meneja wa TRA mkoa wa Ruvuma Rozalia Mwenda alisema kuwa ofisi yake kwa kushilikiana na wafanyabiashara bado inahitaji kuwa na ushirikiano mkubwa kwa lengo la kuendelea kukusanya kodi ya serikali na si vinginevyo.
MWISHO
Chapisha Maoni