Wanachuo wa Veta ya Chang'ombe kilichopo Jijini Dar Es Salaam wakiwa kwenye mafunzo halisi ya ufundi magari |
Wanachuo wa chuo cha Veta wakiwapokea wakufunzi na wageni mbalimbali ambao hawapo pichani kwenye viwanja vya chuo cha chang'ombe |
Gari ambalo lim,etolewa na USAID kwa ajiri ya mradi wa mafunzo kwa watoto wanaoishi mazingira magumu |
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WANAFUNZI wa
kozi ya ufundi magari na udereva katika chuo cha Mafunzo ya ufundi stadi Veta
Songea wametakiwa kuvitunza vitu vyao vya kujifunzia ili viweze kuwasaidia
katika upatikanaji wa mafunzo na kuviacha salama ili viweze kuwasaidia na
wanafunzi wengine
Wito huo
umetolewa jana kwenye viwanja vya Veta mjini hapa na Mkurugenzi wa
International Youth Foundation(IYS) Saraha Shebehe wakati wa hafla fupi ya
kukabidhi magari mawili kwa ajiri ya chuo cha Veta cha Chang’ombe na Songea yenye
thamani ya zaidi ya milioni 250
Shebehe
alisema kuwa mradi wa kutoa kozi fupi kwa watoto wanaoishi katika mazingira
magumu kwenye vyuo hivyo Tanzania Youth Scholars unafadhiriwa na shirika la
misaada la Marekani(USAID) kupitia shirika la IYF unalengo la kuwakomboa vijana
wenye mazingira magumu
Alisema kuwa
lengo la kutoa msaada wa magari hayo ni kuwawezesha Veta ambao ndio wadau
wakubwa wa utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi kufundisha vijana wengi zaidi
ili waweze kujiajiri au kuajiriwa kwenye soko la ajira baada ya kuhitimu
mafunzo yao
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkuu wa chuo cha Veta Songea Gidion Nairumbe alisema kuwa
mwanzoni mwa mwezi April mwaka 2014 chuo cha Veta Songea kikishirikiana na
Ofisi ya Veta kanda ya Nyanda za Juu kilitoa wazo la kuwasaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu ya mafunzo ya ufundi stadi
katika kozi fupi
Nairumbe
alisema hadi sasa mafunzo hayo yametolewa kwa awamu moja na awamu ya pili
yanaendelea na wanufaika ni kutoka wilaya ya Songea vijijini na mitaa iliyopo
pembezoni mwa Manispaa ya Songea
Alisema katika
mradi huo wanafunzi hao wameweza kupata mafunzo yatakayowasaidia kujiajiri,kupata
mafunzo ya ujasiliamali na kuunda vikundi vya ujasiliamali na kupatiwa vifaa
vya kufanyia shughuli za ujasiliamali kulingana na fani walizosomea
MWISHO
Chapisha Maoni