NA, STEPHANO MANGO,SONGEA
VIJANA 132 waishio
katika mazingira magumu kutoka wilaya ya Songea Mjini na Songea Vijijini katika
Mkoa wa Ruvuma wamepata ufadhiri wa mafunzo kwenye chuo cha Veta Songea katika
fani mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho
Akizungumza na wazazi na walezi wa vijana hao jana kwenye
ukumbi wa Veta Mjini hapa Meneja mradi wa Tanzania Youth Schoolar Project (TYS)
Iris Kilayo alisema kuwa lengo mradi huo unasimamiwa na International Youth Foundation
kuwasaidia vijana kupata mafunzo stadi muhimu katika chuo cha Veta Songea
Kilayo alisema kuwa mradi huo wa awamu ya pili utatoa
mafunzo na kusimamia ufadhiri husika ili
kuwasaidia kupata ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri baada ya
kuhitimu mafunzo yao katika fani mbalimbali
Alisema kuwa lengo kubwa ni kupunguza idadi ya vijana wanaojiingiza
katika vitendo viovu vya umalaya, utapeli, wizi na matumizi ya madaya ya
kulevya ambako kunawaathiri vijana wengi na kusababisha upotevu wa nguvu kazi
ya taifa
Alifafanua kuwa Mradi huo unawajibika kuwagharamia vijana
hao kuwalipia ada, kuwapatia nauri za kuja chuoni na kurudi nyumbani kuwanunulia
sare kwa maana ya viatu, tisheti,overall pamoja na viandikio
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Veta Gideon Ole Nairumbe
alisema kuwa mwaka jana kupitia mradi huo ulifanikiwa kutoa mafunzo kwa vijana
72 na mwaka huu wanatoa mafunzo kwa vijana 60 hivyo jukumu la wazazi
kushirikiana na chuo ili kuweza kufanikisha mafunzo hayo muhimu
Nairumbe aliwataka wazazi na vijana hao kuhakikisha kuwa
wanaendeleza nia njema ya mradi kwa kuhakikisha nyenzo na fedha zinatumika kwa
maslahi mapana yaliyoanishwa kwenye mradi husika ili kuwezesha upatikanaji
stahiki wa mafunzo chuoni hapo
MWISHO
Chapisha Maoni