NA STEPHANO MANGO, SONGEA.
WAGOMBEA Ubunge jimbo jipya la Mdaba wapigana vikumbo kwenye ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Songea vijijini kuchukua fomu na kuzirejesha kuwania nafasi hiyo wakiwemo vigogo wawili mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Glorias Luoga na makumu mkuu wa chuo kikuu cha
Ardhi mipango fedha na utawala Profesa Eleuther Mwageni.
Vikumbo hivyo vimejitokeza vya makada wa chama cha Mapinduzi
vimetokea jana kwenye ofisi ya CCM ya wilaya ambako wagombea hao walifika kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ambao kila mmoja aliongozana na wapambe wake.
Kada wa kwanza ambaye alifika kwenye ofisi za chama hicho huku akiwa amesindikizwa na wapambe wake majira ya saa 4 asubuhi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Tarime Luoga alichukua fomu na kuijaza kisha akairejesha ndani ya dakika 30 ambapo baadaye aliongea na waandishi wa habari na kueleza sababu zilizomsukuma kuwania nafasi hiyo.
Luoga alisema kuwa amelazimika kujitolea kuja kuungana na wananchi wa jimbo jipya la Mdaba katika kuhakikisha kuwa maendeleo yao yanafanikiwa katika kuboresha miundombinu ya barabara ,Shule za msingi,Sekondari ,Zahanati na Vituo vya afya pamoja na kuhakikisha wananchi wanajengewa makazi bora.
Naye Profesa Mwageni muda mfupi baada ya Luoga kuondoka alitinga ofisi za CCM akiwa ameongozana na wapambe wake na alichukuwa fomu ambayo baada ya masaa mawili kupita aliirejesha na kisha aliongea na waandishi wa habari ambapo alieleza kuwa kutokana na uchungu aliyonao
kwa wananchi wa jimbo la madaba ameamua kuchukua fomu ya kugombea
ubunge ili awe muwakilishi wa jimbo hilo ambalo limekuwa na changamoto
nyingi zinazotakiwa kutatuliwa na kiongozi ambaye ni makini.
Hata hivyo alisema kuwa kwa sasahivi ni mapema mno kuelezea
vipaombele vya utekelezaji ila endapo akifanikiwa kushinda nafasi hiyo
ya ubunge atacheza na irani ya chama cha Mapinduzi ambayo
inayotarajiwa kutolewa kwa siku hizi za karibuni.
Kwa upande wake Joseph Mhagama ambaye ni mkurugenzi wa asasi isiyo ya
kiserikali RUCODIO wakati akichukua fomu mbele ya katibu wa chama cha
Mapinduzi wilaya hiyo Rajabu Uhonde alisema kuwa kwa muda mrefu
amekuwa akishirikiana zaidi na wananchi kwa kuanzisha miradi
mbalimbali kwa wakulima wadogo ikiwa ni pamoja na kilomo cha
ufuta,Alizeti na Tangawizi hivyo ameahidi kuwa endapo atakuwa mbunge
wa jimbo hilo wananchi wataboreshewa uchumi wao tofauti na hivi sasa.
Alifafanua zaidi kuwa Halmashauri ya Madaba ina jimbo jipya na
inawanchi ambao wanavipato vidogo hivyo wanahitaji kujengewa uwezo
zaidi ambao utamfanya kilamwananchi ambaye ni mkulima kuwa na kipato
cha kiasi kichopungua shilingi ,300,000kwa mwezi.
WAKATI huo huo mtoto wa katibu mkuu wa zamani wa chama cha Mapinduzi
marehemu Dr.Lawrence Mtazama Gama ,Musa Gama ambaye alikuwa mkuu wa
kitengo cha mawasiliano biashara na uchumi katika benki ya biashara ya
China iliyopo jijini Dareselaam majira ya saa za asubuhi alitinga
kwenye ofisi za chama cha Mapinduzi wiya ya Songea mjini kwa aajili ya
kurudisha fomu ya kuwania ubunge wa jimbo la Songea mjini.
Gama alisema kuwa mambo matatu yaliyomsukuma kuchukua fomu ,kwanza ni
haki yake ya msingi kama watanzania wengine ambao wanataka kuwania
nafasi hizo,mbili Thamira imemtuma kuona umhimu wa kurudi nyumbani
Songea kushirikiana na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo
kwa kuboresha huduma mbalimbali za jamii.
MWISHO.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni