RC WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKIZUNGUMZA JAMBO
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa
Kilimanjaro Leonidasi Gama amemmwagia sifa mgombea Uraisi kipitia chama cha
Mapinduzi Dr.John Pombe Magufuli kuwa anastahili kuwaongoza watanzania kwani
Dr. Magufuli ni tingatinga ambalo linauwezo wa kuwaweka mahali pazuri
watanzania na si vinginevyo.
Gama alimwaga
sifa hizo juzi majira ya saa za mchana kwenye mikutano ya kampeni ya kuwania
ubunge kupitia chama hicho katika jimbo la songea Mjini iliyofanyika kwenye
kata za Mwengemshindo na Ruhuwiko.
Alisema kuwa ni
vyema wananchi wakiwemo wanachama wa ccm wakaona umuhimu wa kumchagua Dr.
Magufuli ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano.
Alifafanua
zaidi kuwa Dr. Magufuli ambaye ni waziri wa ujenzi amefanya kazi kubwa sana
hapa nchini ya kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya barabara hapa nchini inapitika
kwa urahisi kwani barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha Lami.
Aidha Gama
ambaye ni mgombea kati ya wagombea 8 wa ubunge kwenye jimbo la songea mjini
amesema kuwa anaomba kuwa mwakilishi wa wakazi wa manispaa ya songea kwenye
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaniendapo atafanikiwa kuwa mbunge atafanya
kazi kama Greda linavyotengeneza barabara na kwamba madiwani watakaochaguliwa
kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (ccm) watakuwa ni sawa na mitambo ya
kushindilia.
Alieleza zaidi
kuwa anataka atumie uwezo wake alionao katika kuboresha maendeleo mbalimbali
ndani ya manispaa ya songea na wananchi waondokane na kero wanazokabiliana nazo
na kwamba amedai kuwa anaumia sana baada ya kusikia kero za wakulima ambao
wengi wao wanajitahidi kulima mahidi lakini wanapotaka kuyauza wanaambiwa kuna
tatizo kubwa la soko la mahindi.
Amewaomba
wananchi wa songea kuwa siku itakapofika ya uchaguzi kura ya kwanza wahakikishe
wanaipeleka kwa tingatinga Dr. Magufuli ambaye ni mgombea wa urais kupitia ccm
na kula ya pili wahakikishe wanaipelekwa kwenye greda ambaye ni Leonidasi Gama
na kula ya tatu wawachague madiwani wa ccm ambao ni mitambo ya kusindilia ili
kuleta maendeleo ya watanzania.
Kwa upande wake
mhaziri wa chuo kikuu cha ufund i
tawi la Mbeya Erick Mapunda aliwaomba wananchi wamchague kuwa mwakilishi wao
Bungeni kwani ameamua kwa dhati kurudi nyumbani kufanya kazi na wanasongea
pamoja na kuhakikisha changamoto zilizopo za migogoro ya ardhi na fidia
wanazodai baadhi ya wananchi wa eneo la mwengemshindo ataweza kuzishughulikia
ili waweze kupatiwa fedha wanazodai kwenye mradi uliotengwa kwenye eneo hilo
kwa ajili ya viwanda wa (EPZA).
Mkuu wa wilaya
ya Hanang Peter Miti wakati alipopewa nafasi aliwaomba wananchi waone umuhimu
wa kuwachagua kuwa mbunge wao na endapo watafanikiwa atahakikisha kuwa soko la
mahindi linakuwa wazi tofauti na hivi sasa wakulima wamekuwa wakirubuniwa na
walanguzi ambao wamekuwa wakinunua mahindi kwa bei ya chini tofauti na
uzalishaji wa zao hilo.
Naye mbunge wa
viti maalumu kupitia vyuo vikuu Dr. Theresa Uviza alisema kuwa akiwa waziri wa
mazingira alionyesha umuhimu mkubwa kwa wakazi wa manispaa ya songea wa kuwa
karibu nao ambapo alifanikisha hospitari ya serikali ya mkoa wa songea kupata
vifaa mbalimbali vya tiba pamoja na vitanda vya kulalia wagonjwa hivyo endapo
wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao watapata manufaa zaidi kwa kuwa
myanya ya kupata misaada zaidi anaijua.
Katibu wa ccm
wa wilaya ya Namtumbo Azizi Mohamed Fakil amesema kuwa wananchama wa chama cha
mapinduzi wakiwemo mabarozi wanaishi na kufanya kazi kama makalai hivyo endapo
atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la songea mjini atahakikisha kuwa tatizo hilo
linaondolewa na ofisi zote za matawi na kata
ambazo majengo yake yapo katika hali mbaya yatafanyiwa matengenezo
tofauti na ilivyo sasa.
MWISHO
Chapisha Maoni