RPC RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
Na Stephano Mango, Mbinga
MWANAFUNZI wa darasa la 5 katika shule
ya msingi Mahela iliyopo eneo la Ruhuwiko Mbinga mjini Frank Hyera (15)
amefariki dunia baada ya kupigwa na jiwe kichwani na mwanfunzi mwenzake.
Akizungumza na www.mangokwetu.blogspot.com jana ofisin
kwake Kamanda wa polisi mkoa wwa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo
lilitokea agost 3 mwaka huu majira ya saa saba mchana huko katika mtaa wa Matarawe
uliopo Ruhuwiko Mbinga ambako Hyera alipigwa jiwe kichwa na mwanafunzi mwenzake
Victor Komba (9).
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku
hiyo ya tukio Komba anayesoma darasa la 3 katika shule ya msingi Mahela
alimpiga jiwe Hyera wakati wanacheza kwenye eneo la shule hiyo.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kutokea tukio
hilo Hyera alipoteza Faham na baadaye alikimbizwa katika hosipitali ya srikali
ya wilaya ya mbinga kwa matibabu zaidi lakini siku ya kuamkia agost 4 mwaka huu
majira ya saa sita na robo usiku mtoto huyo Hyera alifariki Dunia.
Kamanda Msikhela alisema kuwa hata
hivyo jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia Komba kwa usalama wa maisha yake
na upelelezi bado unaendelea kuhusiana na tukio hili.
MWISHO

Chapisha Maoni