NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WATU wasiofahamika ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa vyama
vya upinzani wamebomoa mashina mawili ya chama cha mapinduzi CCM pamoja na kuchana bendera kisha kunyea mavi na kuyachana mabango ya wagombea wa chama hicho
yaliyokuwa yamebandikwa katika mtaa wa Makambi kata ya
Ndilimalitembo Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma.
Akiongea na Mtandao huu jana Katibu wa CCM wa tawi la
Makambi [B],Paris Mauwa alisema tukio
hilo limetokea juzi usiku katika eneo hilo baada ya watu hao kufanya vitendo hivyo vya kubomoa mashina
pamoja na kuchana bendera na mabango.
Mauwa alisema kuwa
kufuatia tukio hilo chama kilikwenda katika ofisi za polisi na kutoa taarifa ya
uharibifu huo na kisha kupata ,RB yenye NA,SONG/IR/4006/2015 ili kufanikisha
kuwatafuta wanaofanya vitendo hivyo vya
uharifu maana ni kinyume na sheria za uchaguzi.
Alisema kuwa licha ya
kuyachana mabango ya wagombea kuanzia nafasi ya Urais hadi udiwani watu hao
walichana bendera na kuwekea kinyesi kwenye bendera jambo ambalo alidai kuwa
inaonyesha kuwa ni wafuasi wa vyama vya upinzani kwa kuwa kata hiyo
wanashindania watu wa vyama vitatu katika ngazi ya udiwani ambao ni Cresensia
Kapinga wa CCM,Leonadi Miholo wa chadema,Yusuphu Kanduru wa ACT Wazalendo.
Baadhi ya wakazi wa
eneo hilo ambao hawakutaka kutaja majina yao wakiongea na Mtandao huu walisema
kuwa wanasikitishwa na vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watu kulingana na ukeleketwa wa vyama
vyao na kuwafanya wakiuke sheria za uchaguzi.
Walisema kuwa kuchana
mabango ,bendera pamoja na kubomoa mashina
ya vyama hamanishi kuwa unashawishi ushindi kwenye chama chako bali ni
wapigakura ndiyo wenye maamuzi sahihi ya kumchagua mgombea wanayemtaka.
Kwa upande wake
kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Revokatus Malimi amesikitishwa na
kitendo kilichofanywa na watu wasiyokuwa na nidhamu kwa kuharibu mashina ya chama
cha mapinduzi ,kuchana bendera za chama hicho ,mabango na kuweka vinyesi jambo
ambalo amedai kuwa ni kosa la jinai hivyo jeshi la polisi kupitia kitengo
iterejesia limeanza kufanya msako mkali wa kuwabaini wahalifu hao.
Chapisha Maoni