Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Walimu wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo lao
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WALIMU kipitia chama
chao cha Walimu mkoani Ruvuma (CWT) wamepaza sauti zao kwa lengo la kuunga
mkono taarifa ya chama cha walimu Tanzania
(CWT) iliyotolewa na rais wa chama hicho Gratian Mukoba kuhusu serikali kuto
tekeleza kwa wakati madai mbalimbali ya walimu na kupuza malalamiko yao.
Hayo yamesemwa jana na
mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma (CWT) Beno Mwenda wakati
akizungumza na waandishi wa habari mbele
ya watendaji wakiwemo makatibu wa
wilaya na mkoa kwenye ofisi za chama hicho.
Mwenda alisema
kuwa muundo mpya wa utumishi wa walimu
waraka namba mbili wa mwaka 2014 uliwaagiza waajili wote wakiwemo wakurugenzi
watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa
kuwaandikia barua watumishi wote wakiwemo walimu za kuonyesha mabadiliko
ya majina ya vyeo kuanzia July 1, 2014.
Alieleza zaidi kuwa
katika mkoa wa Ruvuma ni mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya songea ambaye
ndiye ametekeleza kwa kuwaandikia walimu wachache japokuwa zinamakosa
yanayohitaji marekebisho ambapo wakurugenzi wa wilaya za Songea, Mbinga, Nyasa,
Namtumbo na Tunduru wamekaidi kutekeleza maagizo ya walaka huo hivyo kuwafanya
walimu wote waichukie serikali yao.
Alifafanua zaidi kuwa
walimu wakongwe waliogota TGTS E,F,H na kutopandishwa madaraja ilipofika July
1, 2015 serikali iliahidi kuwapandisha madaraja walimu wote waliogota july 1, 2015 badala ya
july 1, 2014 kama waraka ulivyokuwa unahitaji hivyo kwa mkoa wa Ruvuma hakuna
mkurugenzi aliyetengeneza bajeti kwa ajili ya kuwapandisha madaraja walimu hao
waliogota TGTSE ni 2608, TGTSF ni 223, TGTSH ni 18 na TGTS1 ni 4 kwa hiyo jumla
ya walimu 2855 waliogota wamenyimwa
kupewa madaraja mapya.
Alisema kuwa pia
kuwaingiza wakaguzi wakuu wa shule wa wilaya na kanda katika muundo wa
mishahara ya viongozi wa serikali na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule za
msingi, sekondari, wakaguzi wa kata na wakuu wa vyuo vya ualimu serikali ilitoa
waraka namba 3 wa mwaka 2014 ulioagiza kwamba utekeleza wake uanze July , 2015
jambao ambalo halijatekelezwa.
Hivyo mwenyekiti wa chama hicho mkoani Ruvuma Mwenda ameitaka serikali ihakikishe kuwa madai
mbalimbali ya walimu ambayo tayari yamehakikiwa
yalipwe haraka iwezekanavyo na kwamba wakurugenzi wa halmashauri ambao
wanadaiwa walitumia fedha zilizotakiwa kuwalipa walimu madai yao wahakikishe
kuwa wanazirejesha haraka na kuwalipa walimu husika kabla chama cha walimu(CWT)
hakijawachulia sheria kali na serikali pia iheshimu na kutekeleza waraka namba
3 wa mwaka 2014 kuhusu mishahara pamoja na posho ya madaraka pamoja na viongozi
wa elimu kwa kuwatambua wakaguzi wakuu wa wilaya, kanda waliopo wenye sifa
kuwalipa mishahara viongozi wa serikali LSS(E) na kuwaendeleza wasio na sifa na
si vinginevyo
MWISHO

Chapisha Maoni