NICHAGUENI
NITIMIZE DHANA YA WANAWAKE NA UONGOZI-JENISTA MHAGAMA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
DHANA ya wanawake na uongozi kwa kabila la Kingoni lilianza toka zamani wakati wa utawala wa kichifu ambapo kwa eneo la mkoa wa Ruvuma kulikuwepo na Chifu mwanamke aliyetambulika kwa jina la Mkomanile na mpaka sasa wanawake ndio viongozi wa maisha ya kila siku kwenye jamii zetu
Kwa
upande wa nafasi za uongozi wa kisiasa toka mfumo wa vyama vingi uanze takwimu
zinaonesha kwamba mwaka 1995 wakati uchaguzi wa vyama vingi uliporejeshwa ni
wanawake wachache sana walijitokeza kugombea.
Katika uchaguzi wa mwaka huo ni wanawake wanane tu waliofanikiwa kushinda viti vya ubunge kwenye majimbo na wengine 37 wakitoka kwenye Ubunge viti maalumu . Hiyo ikafanya idadi ya wabunge wanawake kuwa 45 kati ya wabunge 269 waliochaguliwa. Takwimu zinaonesha wabunge wameongezeka kutoka asilimia 16 mwaka 1995 hadi asilimia 36 mwaka 2010
Majimbo yaliyopo Mkoa wa Ruvuma ni 9 na katika hayo ni majimbo mawili pekee ndio yanayogombewa na wanawake ambapo kwenye jimbo la Peramiho anagombea Jenista Mhagama na Jimbo la Nyasa anagombea Mhandisi Stella Manyanya
Nimebahatika kuzungumza na Mwalimu mstaafu Ching’ang’a Mabel ambaye alimfundisha Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama shule ya Msingi Mfaranyaki miaka ya 1978 alisema kuwa anamfahamu Jenista kwa karibu sana kwani amelelewa kimaadili ya kabila la kingoni
Mabel alisema kuwa familia ya Mzee Joakim Ngonyani na Mama Epifania Shawa(Mungu awarehemu) ambao ni wazazi wa Jenista walikuwa jilani sana na familia za kichifu hivyo Mama mzazi wa Jenista amezaliwa ukoo wa machifu akina Gama na akina Shawa Jenista amerithi uongozi wa kikabila la kingoni na ndio maana amekuwa akipata baraka za kiuongozi na kweli anawatumikia wananchi kiukamilifu
Alisema kuwa wakati huo toka akiwa shule ya msingi Jenista na wenzake walikuwa ni hodari wa kula vyakula vya kienyeji (kimila) na alikuwa mshiriki mzuri sana wa sherehe na misiba ambapo alikuwa anavaa nguo za asili kwani kwenye shughuli za kingoni ni lazima ngoma za asili na vyakula vya asili vipikwe na ilikuwa ngumu sana kuvaa nguo za kigeni kwani kulikuwa na utamaduni mzuri wa kiasili
Alifafanua kuwa Jenista alipokuwa shuleni au kwenye michezo muda wote alikuwa ni mcheshi na alikuwa ni msichana wa kuigwa na ndio maana alianza uongozi toka akiwa shule hali ambayo ilimuongezea ujasiri na kujifunza kutoka kwa wenzake
Nimebahatika leo kushuhudia namna anavyoshirikiana na wenzake pamoja na wananchi kuleta maendeleo katika jimbo lake kwani tofauti inaonekana kabla yeye ajawa mbunge na leo alivyo mbunge kwenye jimbo la Peramiho
Kwa
kuwa uongozi ni kuonyesha njia na kutembea na wananchi katika njia hiyo ili
kufikia malengo stahiki katika jamii husika, nashawishika bila shaka kuwaomba
wananchi wa jimbo la Peramiho octoba 25 mwaka huu wajitokeze kwa wingi
kumchagua Jenista Mhagama kuwa mbunge wa jimbo hilo kwani kwa aliyoyafanya
anatosha kuchaguliwa tena
“Sisi wanawake tuna uwezo tena pengine kuliko baadhi ya wanaume ila tunaangushana wenyewe kwa wenyewe kutokana na kutoungana mkono pale ambapo miongoni mwetu tunapogombea nafasi mbalimbali kwa kutoaminiana wenyewe”alisema Mabel
Akizungumza kwenye mikutano yake ya kampeni za kujinadi na kuwanadi madiwani na mgombea Urais kupitia Ccm kwenye kata za Matimila, Litisha, Ndongosi na Kilagano Jenista Mhagama alisema kuwa wanaperamiho wanayofursa nzuri ya kutafakari na kuuthamini utamaduni na mila zetu ili ziweze kutuletea kipato
Mhagama alisema kuwa mila,desturi na lugha ya kingoni ikichambuliwa vyema na kupangwa na kusambazwa kikamilifu inaweza kubadili kwa kiasi kikubwa hali za kiuchumi za wananchi wa jimbo la Peramiho na viunga vya jilani kwa kuingiza fedha za kigeni
“Naombeni mnichague tena niwe mbunge wenu ili niweze kufanikisha hilo kwani kwa miaka 10 ya uwakilishi wangu nilijikita kujenga miundominu muhimu kwenye masuala ya elimu,afya, kilimo, utawala bora, miundombinu ya ujenzi na barabara, kiuchumi na kijamii” alisema Mhagama
Alisema kuwa leo kuna utandawazi wa kiutamaduni ambapo utamaduni wenye nguvu ndio hujisambaza na kuutawala ule usio na nguvu kutokana na maingiliano ya tamaduni mbalimbali, hivyo tutumie fursa ya utandawazi kuulinda utamaduni wetu ili utupatie fedha za kigeni
Alisema kuwa Jimbo la Peramiho lilikuwa kubwa sana ambapo bajeti yake ilikuwa ndogo hivyo kitendo cha kuligawa na kupatikana kwa jimbo na wilaya ya madaba kutawezesha kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto zilizobaki kwa kipindi cha 2015-2020
Nilijitahidi sana kupigania utatuzi wa changamoto husika na kufanikiwa kuzitekeleza kwa kiasi kikubwa na kuwafanya wananchi waendelee kunufaika na uwakilishi wangu bungeni na Serikalini kwani wakati naingia kwa mara ya kwanza hali ya jimbo hilo ilikuwa kwa sekta zote ilikuwa ni taabani
Kwasasa
jimbo hilo lenye kata 16 ikiwemo ya Matimira ,Kilagano ,Ndongosi,
Mpandangindo, Mbinga Mhalule, Mtyangimbole, Matumbi, Gumbiro, Nakahuga
Magagura,peramiho,Mpitimbi,Mhukuru,Maposeni,Parangu,Litisha
Bado zipo changamoto ambazo natakiwa kuzifanyia kazi kikamilifu kupitia ilani na mipango ya serikali kwa kipindi cha 2015-2020 kwenye sekta ya Elimu, afya, nishati ya umeme,maji,barabara na ujenzi,Kilimo na ushirika,mifugo na uvuvi,ardhi na maliasili,biashara na masoko,mawasiliano,uwekezaji, michezo na ajira
Alisema jimbo la Peramiho ni eneo muhimu la kihistoria ya nchi na ya Kanisa katoliki nchini na pia ni kitovu cha utalii wa kihistoria na kiutamaduni hivyo ni muhimu likaendana na historia yake kwa ukombozi wan chi hii na ukristo nchini
Nawaomba wananchi wa Jimbo la Peramiho wanichague tena niwe mbunge wao ili niweze kukamilisha miradi ya kijamii na kiuchumi ambayo tumeianza na kuiendeleza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya barabara, ujenzi, maji, afya na uwezeshwaji wa kiuchumi kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi
Nakusudia kuongeza zahanati moja moja kila kata na nyumba za waganga na wauguzi na kuziwekea umeme jua kama umeme wa vijijini (REA) haujaunganishwa kwenye maeneo hayo ili wananchi wasipate tabu ya kufuata huduma, pia nakusudia kushirikiana na Serikali kuongeza vituo vya afya kwani vilivyopo havikidhi idadi ya wananchi ambao wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali
Kwa upande wa sekta ya miundombinu nawajibika mara nitakapochaguliwa tena ni kujenga barabara za kuunganisha vijiji vyote vya jimbo la peramiho na kuimarisha barabara za mashambani hizo ili zipitike muda wote na kuwafanya wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo
Pia kwa upande wa sekta zingine kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi wa Jimbo la Peramiho Ilani ya Chama cha Mapinduzi(Ccm) na Serikali imetoa miongozo stahiki ambayo inatakiwa itekelezwe kikamilifu na kwakuwa mengine mengi nimekwisha yafanya basi changamoto zilizobaki nitazifanyia kazi ili tuiendeleze Peramiho kwa kasi kuongeza uchumi kwa kujenga viwanda na kuanzisha mazao mengine ya biashara na kuwapa mikopo vijana, akina mama na wazee
Ni dhahiri Peramiho ya sasa inaridhisha kwenye sekta zote kwani mwanga wa maendeleo na huduma kwa wananchi unaonekana kweupe, hivyo wananchi wa Peramiho wanatakiwa wampate mwakilishi mwenye ndoto za maendeleo ambaye ni Jenista Mhagama
Wanaperamiho wanatakiwa wasibweteke na maendeleo yaliyopatikana toka 2005 hadi 2015 hivyo wanatakiwa waanze upya na Jenista Mhagama ili kuifikia ndoto za kuifanya peramiho iwe ni eneo la mfano kwa maendeleo kwa mkoa wa Ruvuma na Taifa kiujumla
Uvumilivu ni kushikiria jambo mpaka mafanikio stahiki yapatikane na kipimo cha mafanikio ni vikwazo vya kuyafikia maendeleo kusudiwa hivyo ni muhimu kuanza upya kwa kuweka vipaumbele na kufanya maamuzi mazito, makubwa na ya haraka kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi
Mahitaji ni mengi na rasilimali ni chache kwa wakati mmoja kwani katika maisha ni lazima kufanya gharama ya hiari ya kuangalia lipi lianze na lipi lisubiri na kwa wakati gani na kwa kuwa jimbo la Peramiho limegawika ni jambo la busara ambalo linapaswa lipongezwe kwani kiutawala ukubwa wa majukumu, raslimali na kijografia umepungua, hivyo tunaishukuru Serikali kwa kugawa jimbo na Halmashauri ya Wilaya ya Songea na kupatikana Jimbo la Madaba na Halmashauri yake
Inahitaji fikra sahihi, dira na maamuzi mazito kutekeleza mahitaji ya mtu binafsi na mahitaji ya Jamii nzima hivyo ni lazima kiongozi na waongozwa wakubaliane vipaumbele na wafikie maamuzi na sio kulaumiana kwani sote tunahitaji maendeleo
Nakubaliana na Jenista mhagama katika mipango yake ya kuanza upya kuiondoa Peramiho hapa ilipo na kuipaisha katika sekta za utalii,kilimo,masoko,ardhi,miundombinu,nishati na madini,afya,elimu, mawasiliano na utawala hivyo anafaa kuchaguliwa
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana kwa 0715-335051
Anapatikana kwa 0715-335051
MWISHO
Chapisha Maoni