0
              KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA ZUBER MWOMBEJI
 
NA STEPHANO MANGO,SONGEA

WAENDESHA Bodaboda zaidi 200 wakiwa na siraha za jadi mapanga, virungu, shoka, Mundu na Nondo wameyazingira maeneo yote ya eneo la Lizaboni na subira manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa madai kuwa wanamsaka Pengo Majuto amabaye anadaiwa kuhusika na matukio zaidi ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni mjini hapa.

Baadhi ya waendesha bodaboda ambao hawakutaka majina yao yatajwe walisema kuwa kuna matukio mfululizo ya mauaji ambayo yametokea mjini songea na yameonyesha wazi kuwa yanawalenga waendesha bodaboda tu.

Walisema kuwa katika matukio yote ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni waendesha bodaboda wameuwawa kikatili na kundi ambalo inadaiwa linaongozwa na majuto ambalo ni la muda mrefu mjini hapo walieleza kuwa kufuatia kutokea matukio hayo mfululizo ambayo walidai kuwa yamesababisha kuleta hofu kwa waendesha bodaboda mjini Songea wamelazimika kukutana kwa pamoja kwa lengo la kulisaka kundi hilo ambalo linaonesha polisi wameshindwa kulikamata.

Walifafanua kuwa Aprili 18 mwaka huu majira ya saa za usiku kwenye eneo la mtaa wa namanyigu kata ua mshangano manispaa ya songea mwendesha bodaboda Fabiani Aliso Mwakasege mkazi wa moonlight bombambili akiwa amembeba abiria wake ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara  moja waliuwawa na kundi la watu wasiofahamika kwa kukatwa katwa sehemu mbalimbali za mwili  na kitu chenye ncha kali.

Walisema kuwa Aprili 25 mwaka hu majira ya saa 2 asubuhi huko katika mtaa wa Muungano eneo la mkuzo kata ya Msamala pia mwendesha bodaboda aliuwawa na kundi la watu wasio fahamika kisha walipora pikipiki aliyokuwa akiiendesha jambo ambalo liliendelea kuleta hofu kwa waendesha bodaboda na kwamba kati ya Aprili 26 na 27 mwaka huu kuna matukio mawili mwengine yametokea kwenye maeneo ya subira na mjimwema ambako waendesha bodaboda waili tofauti waliuwawa kwa kukatwakatwa sehemu mbalimbali  na kitu chenye ncha kali na kundi la watu wasio fahamika na kuwanyanganya pikipiki walizokuwa wakiziendesha.

Wameliomba jeshi la polisi kufanya dolia ya nguvu ya kuwasaka watu wabaya ambao wamekuwa wakiwaua waendesha bodaboda ikiwa ni pamoja na kumkamata  Pengo majuto ambaye anadaiwa kuonekana katika baadhi ya mitaa ya mjini hapa lakini polisi wameshindwa kumpata.

Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Yahya Athumani alipohojiwa na gazeti hili kuhusiana na kuwepo kwa mauaji ya waendesha bodaboda alikiri kutokea na alidai kuwa kwa hivi sasa Polisi inawashikilia waatu wawili wanaodaiwa kuhusika na unyanganyi wa pikipiki katika maeneo ya songea mjini.

Alifafanua kuwa Polisi imejitahidi kulizuia kundi kubwa la waendesha bodaboda waliyokutwa kwenye maeneo ya Lizaboni na Subira ambao walikuwa wakidai kuwa wanamsaka majuto na kwamba kwa sasa hivi wameshauriwa wawe wavumilivu wakati askari polisi wakiendelea kufanya uchunguzi zaidi ili kuubaini ukweli halisi wa matukio hayo.

MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top