NA CRENCENSIA KAPINGA,SONGEA
JESHI la Polisi Mkoa wa
Ruvuma linamshikilia Zainab Dotto Yusuph (35) Mkazi wa Kitongoji cha Chalinze
Kilichopo kata ya Mawenzi Tarafa ya Nakapanya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma
kwa tuhuma za kumkata mume wake Patrick Mlowa(60) uume na korodani na kumsababishia
maumivu makali
Habari zilizopatikana jana
mjini hapa ambazo zimethibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela zimesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya 9:12 usiku huko
katika eneo la Majimaji lililopo katika kitongoji cha Chalinze ambako Mlowa
alikumbwa na mkasa huo
Kamanda Msikhela alisema
kuwa Inadaiwa Mlowa alijeruhiwa vibaya kwa kukatwa na kisu viungo vyake vya
sehemu za siri baada ya kuwepo ugomvi wa muda mrefu na mke wake kutokana na
wivu wa kimapenzi
Alisema kuwa inadaiwa
baada ya kukatwa sehemu zake za siri majirani walimsikia akilia kwa sauti huku
akigugumia maumivu makali ambayo alikuwa akiyapata na walipofika kwenye eneo la
tukio walimkuta akiwa amelala huku viungo vyake vikiwa vinanin’ginia baada ya
kukatwa na nyingi zikiwa zimetapakaa kwenye eneo la tukio
Alieleza kuwa majirani hao
wakisaidiana na viongozi wa Serikali ya Kijiji walitoa taarifa kwenye kituo cha
Polisi Wilaya ya Tunduru na baadae walimkimbiza Mlowa kwenye Hospital ya
Serikali ya Wilaya ya Tunduru ambako amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu
Alieleza zaidi kuwa chanzo
cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi uliopo miongoni mwao na Jeshi la Polisi
Tayari limeshamkata Zainab na kwamba upelelezi unaendelea na ukikamilika
atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili
MWISHO
Chapisha Maoni