NA STEPHANO MANGO.SONGEA
MTU mmoja amefariki dunia
papo hapo na wengine sita wamejeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa
wakisafilia kugongana uso kwa uso na gari nyingine huko katika la Kijiji cha
Sanangura nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa kwenye barabara ya kutoka
Songea kwenda Njombe
Akizungumza na Gazeti hili
Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema tukio
hilo lilitokea februari 20, mwaka huu majira ya saa 9:40 usiku ambapo alimtaja
aliyefariki dunia kuwa ni Sista Innoncensia Kisaka(33) wa kanisa katoliki jimbo
la Iringa
Kamanda Msikhela amewataja
waliojeruhiwa ambao kwa sasa hivi wamelazwa katika Hospital ya Misheni ya
Peramiho kuwa ni Fr Jastin Sapila(70), Sista Christine Banda(63) Sista Karomere
Mfuse(48) Erasto (20) Karo Mhagama(21) na Thadei Charles(20) wote wakazi wa
Seminari kuu Peramiho
Alieleza kuwa Inadaiwa
siku hiyo ya tukio gari lenye namba za usajiri T.94 DDC aina ya Land Cruiser
ambayo ilikuwa inaendesha na Fr Kastori Goriama(52) wa Seminari kuu ya Peramiho
ilikuwa inatoka Iringa kwenda Peramiho iligongana uso kwa uso na gari lenye
namba za usajiri T 926 CDB aina ya Suzuki Carry iliyokuwa inaendeshwa na
dereva ambalo jina lake halikuweza
kufahamika mara moja baada ya kukimbia mara baada ya ajari kutokea ikitokea
Peramiho kwenda Mlilayoyo
Alisema kuwa baada ya
magari hayo kugongana majeruhi sita walikimbizwa katika hospital hiyo kwa ajiri
ya matibabu na kwamba hali zao zinaendelea vizuri na chonzo cha ajari hiyo
kinaendelea kuchunguzwa na kwamba juhudi za Polisi zinaendelea ili kumnasa
dereva aliyekimbia ili hatua za kisheria zichukuliwe juu yake
MWISHO
Chapisha Maoni