0

                                   HAYA NDIYO MIONGONI MWA MAHINDI

NA, STEPHANO MANGO, SONGEA
SERIKALI kupitia wizara ya kilimo  chakula na ushirika imesema kuwa dawa ya deni ni kulipa hivyo tayari kwa awamu ya kwanza  imeanza kuwalipa wakulima wadogo wadogo waliokuwa wameuza mahindi yao kwa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NRFA) Kanda ya Songea kwa msimu uliopita.

Hayo yamesemwa jana kwa nyakati tofauti na waziri wa kilimo chakula na ushirika Steven Wasira wakati alipofanya zihara ya siku mmoja ya kutembelea na kukagua maghala yaliyosheheni mahindi yaliyoko katika vijiji vya Namabengo, Wilayani Namtumbo na kijiji cha Mgazini kilichopo Wilaya ya Songea vijijini.

Alisema kuwa nia ya serikali haikuwa mbaya ya kununua mahindi kwa wakulima ambapo kwa sasa hivi ndiyo maaana waliokuwa wameleta mahindi yao NRFA amabao walikuwa wakisubiri malipo yao kwa sasa hivi kwa awamu ya kwanza wameaanza kulipwa wakulima wadogo wadogo, kwa awamu ya pili wataanza kulipwa wakulima waliouza mahindi kuanzia yenye thamani ya shilingi Million 4 hadi Million 10 na awamu ya tatu watalipwa wakulima pamoja na mawakala ambao wameuza mahindi yao NRFA.

Alisistiza kuwa hakuna mkulima yeyote aliyeleta mahindi NRFA akashindwa kulipwa fedha jambo ambalo kwa hivi sasa linapaswa kufuatwa ni utararibu uliowekwa wa malipo kwa wakulima na si vinginevyo.

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea Mogani Mwaipyana alisema kuwa majukumu makubwa ya wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula ni pamoja na kununua, kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula pamoja na kutoa chakula hicho kwa waathirika wanaobainka kwa na upungufu wa chakula kutokana na majanga.

Alisema kuwa pia NRFA uhuza sehemu ya akiba kwa lengo la kuhakikisha kuwa chakula kilichohifadhiwa kwenye maghala kwa zaidi ya mwaka mmoja hakiaribiki na kutoa nafasi ya ununuzi kwa mazao mapya.

Mwaipyana alieleza zaidi kuwa NRFA Kanda ya Songea ni miongoni mwa Kanda 7 za Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula ambayo inahudumia Mkoa wa Ruvuma na kwamba Kanda hiyo ya Songea imekamilisha msimu wa ununuzi wa nafaka kwa mwaka 2014/2015 ambapo awali serikali katika mwaka wa fedha 2014/2015 ilipanga kununua tani laki 2 za nafaka kupitia wakala wa Taifa ya hifadhi ya chakula hivyo katika kanda ya Songea msimu wa ununuzi wa mahindi ulianza Agoust mwaka jana ambapo kanda hiyo ilikuwa na lengo la kununua tani 40,000 za mahindi lakini ziada kubwa iliyozalishwa na wakulima wamahindi imesababishwa kuwepo na chamoto kubwa la soko kwa zao hilo.

Alifafanua zaidi kuwa kutokana na hali hiyo pamoja na kuwepo mlimbikanao wa nafaka katika vituo vya ununuzi vya NRFA serikali iliongeza lengo la ununuzi wa zao hilo kutoka tani laki 2 hadi tani 280 elfu ili kuepuka kuharibika kwa mazao yaliyokuwa yameletwa na wakulima kwenye vituo kwa ajili ya kuuzwa kwa wakala ya hifadhi ya Taifa ya chakula kanda ya Songea ambayo iliyoongezewa lengo la ununuzi kutoka tani 40,000 hadi tani 60,000.

Meneja wa wakala wa Taifa wahifadhi ya chakula (NRFA)  kanda ya Songea Mwaipyana alisema kuwa ofisi yake mapaka januari 30 mwaka huu tayari imepokea shilingi billion 28 ambazo zimetosha kulipa tani za mahindi 46,000 na kwamba kwa hivi sasa inadaiwa shilingi billion 12.7 licha ya kuwa wanaendela na jitihada za kupata fedha zaidi ili kulipa deni hilo.

Mwisho.



Chapisha Maoni

 
Top