PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA WATUHUMIWA WA UGAIDI MAHAKAMANI
NA
STEPHANO MANGO,SONGEA
WATU
sita wanaotuhumiwa kujihusisha na Vitendo vya ugaidi kwa kutegesha na kuripua
mabomu yaliyotengenezwa kwa kienyeji katika matukio matatu tofauti mkoani
Ruvuma wamefikishwa Mahakamani kujibu Mashtaka yanayowakabili huku nje ya
Mahakama hiyo kukiwa na ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi wakiwemo Askari wa
Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU)
Katika
Mahakama hiyo iliyokuwa na ulinzi mkali huku watu wakikatazwa kuzunguka au
kupita kwenye eneo hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa
Ruvuma Simoni Kobelo, mwendesha Mashtaka ambaye ni Wakili Mfawidhi wa Serikali
Toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Kanda ya Songea Silivanus Mkude aliwataja
washtakiwa Mahakamani hapo kuwa ni Juma Omari Kibwana maarufu kwa jina la
Msabila , Mwalimu Yusuph ,Hamza Singano wakazi wa Majengo Halmashauri ya
Manispaa ya Songea, Yasin Mponda Musa maarufu kwa Jina la Kafupi Mkazi wa Eneo
la Ruvuma Manispaa ya Songea,Hasan Mponda na Said Stivin Mhando
Wakili
Mkude alidai Mahakamani hapo kuwa Washtakiwa wote wanakabiliwa na Mashtaka ya
Matatu tofauti yakujaribu kuwaua Askari Polisi wa waliokuwa doria na Askari wa
Kikosi cha Barabara waliokuwepo kwenye eneo la kazi huko katika eneo la
Mshangano Manispaa ya Songea
Alieleza
kuwa inadaiwa kuwa kosa la kwanza la kujaribu kuua, mnamo desemba 25 mwaka jana
huko katika eneo la Mtaa wa Kotazi Majengo watu hao mmoja kati yao alijaribu
kuwarushia bomu lililotengenezwa kienyeji Askari Polisi waliokuwa wanafanya
doria na kabla hajafanikiwa kurusha bomu hilo lilimripukia yeye mwenyewe na
kumsababishia kifo na Askari Polisi wawili kujeruhiwa
Alisema
kuwa shtaka la pili Octoba 27 mwaka jana majira ya saa 10:00 za jioni
lilichimbiwa ardhini bomu la Kienyeji katika eneo la Mshangano kando kando ya
Barabara ya Kutoka Songea na Kwenda Njombe ambalo hutumiwa na Askari wa Usalama
Barabarani kama kituo cha ukaguzi wa magari yanayotoka na kuingia Songea Mjini
kwa lengo la kuwaripua Askari na kabla hawajatimiza adhima hiyo Askari
waligundua na kulitegeua bomu hilo
Alilitaja
shtaka la Tatu ambalo linawakabili kuwa inadaiwa kuwa Septemba 16 mwaka jana
majira ya saa 12:00 jioni kata ya Misufini karibu na Matarawe Mjini Songea
waliwarushia bomu la kutengenezwa kienyeji Askari waliokuwa Kazini na
kusababisha Askari watatu kujeruhiwa
Hata
hivyo kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za kigaidi,
washtakiwa hawakuweza kujibu mashataka yanayo wakabili na kesi hiyo itafikishwa
Mahakamani tena Februari 19 mwaka huu kwa ajiri ya kutajwa na washtakiwa wote
wamepelekwa Mahabusu baada ya kutokukubaliwa dhamana
MWISHO
Chapisha Maoni