Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Ruvuma Isaya Mbilinyi akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti
NA,
STEPHANO MANGO,SONGEA
JUMUIYA
ya wafanyabiashara Tanzania Tawi la Ruvuma imeitaka Serikali Kutoendelea na
Wazo lake la Kukusanya Kodi kwa Asilimia mia mpaka pale mgogoro uliopo
utakapojadiliwa na Bunge na kufikia maamuzi stahiki kwa maslahi mapana ya
Serikali na Wafanyabiashara
Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo Ruvuma Mwilamba Isaya Mbilinyi akizungumza kwenye mkutano jana
uliofanyika kwenye ukumbi wa Songea Club na kuwashirikisha Mamlaka ya Mapato
Tanzania alisema kuwa imeshangazwa na kitendo cha serikali kupandisha kodi kwa
asilimia miamoja huku ikielezwa kuwa ongezeko hilo halilingani na ukuaji wa
uchumi wa nchi,
Mbilinyi
alisema ni vyema mahesabu hayo ya kodi ambayo yalipitishwa na Bunge
yakaangaliwa upya na kufanyiwa marekebisho, ili kuondoa malalamiko ya mara kwa
mara yanayoendelea kujitokeza miongoni mwa jamii ya wafanyabiashara.
Alisema ni kiwango kipi kilitumika na serikali kukokotoa na kuweka ongezeko hilo ambalo ni kubwa, wakati wakijua fika hali ya uchumi wa nchi kwa sasa sio nzuri na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuwaumiza wafanyabishara, hasa kwa wale wenye mitaji midogo.
“Viwango vipya vya ulipaji kodi vilivyowekwa na bunge ambavyo
utekelezaji wake unapaswa kufanyika kuanzia sasa, wamevipokea kwa shingo upande
na kwamba kuna kila sababu kwa waliohusika kupitisha suala hili (Wabunge) waone
ni namna gani wanalifanyia tena upembuzi yakinifu ili kuondoa malalamiko ambayo
yanaendelea kujitokeza kwa nchi nzima” Alisema Mbilinyi.
Naye Katibu wa Jumuiya hiyo Kipara Nziku alisema kuwa kupanda huku kwa kodi ya mapato kunasababishwa na wataalamu husika wa mamlaka ya mapato nchini kutengeneza hesabu za juu bila kushirikisha wadau husika, yaani wafanyabiashara ambao wangeweza kutoa ushirikiano wa karibu kabla ya kupelekwa bungeni.
Nziku alifafanua kuwa katika jambo hili ni sawa na mamlaka hiyo imetumia ubabe, wakati wanatengeneza viwango hivyo vipya na ndio maana leo vinaumiza wananchi na kusababisha kuichukuia serikali yao.
“TRA tumewasikia hapa mkisingizia wabunge ndio walioweka viwango hivi na kupandisha kodi ya mapato, lakini nataka niwaambie ukweli ni kwamba ninyi watu wa mamlaka ya mapato ndio mnao husika katika kuandaa viwango hivi na baadae vinapelekwa bungeni, hapa tusifike mahali tunadanganyana kama watoto wadogo”, alisema.
Alisema
kamwe hatuwezi kulipa kodi hiyo mpaka changamoto za Matumizi ya Mashine za
Kietroniki(EFD) na Ongezeko jipya la kodi litakapofikia muafaka vinginevyo
hatutaweza kufungua maduka yetu
Akijibu hoja za wafanyabiashara hao wa Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ruvuma Apily Mbaruku alisema kilio hiki cha ongezeko la kodi ya mapato ambacho wanakipigia kelele tayari hata kwa mikoa mingine hapa nchini wanakifahamu na kwamba mfumo huu wa sasa wa serikali kuingia kwenye viwango maalum vya ulipaji wa kodi, ulitokana na wafanyabiashara wengi kutokuwa na mazoea ya kutunza kumbukumbu (Vitabu) vya mahesabu ya biashara wanayofanya kwa kila siku.
Mbaruku alisema, viwango vipya vya kodi ambavyo vimewekwa na bunge ni muhimu kuzingatiwa na vianze kutekelezwa mpaka serikali kupitia bunge lake itakapotoa maamuzi mengine.
MWISHO.
Chapisha Maoni